MBINU ZA KIFANI KATIKA RIWAYA YA MZINGILE YA E.KEZILAHABI (1991)
Riwaya ya Mzingile ni riwaya ya
kifalsafa iliyojikita katika swali “nini maana ya maisha Katika kujibu swali
hili mwandishi amemtumia Kakulu aliyezaliwa katika mazingira ya ajabu kwa
kumchora kama neema kwa maana ya kuona kama mkombozi kwa kutatua matatizo ya
njaa na magonjwa. Hata hivyo Kakuru anapoteza maana baada ya watu kuanza
kumpinga hivyo anakimbilia mlimani. Pia kwa kutumia swali nini maana ya maisha
mwandishi anamlika taasisi za dini ambazo kimsingi ndio mhimili wa maadili
zinaposhindwa kudhibitisha hilo kwa viongozi wa dini (mashekhe na mapadri) wanavyokiuka
maadili. Kwa kutumia swali hilohilo pia mwandishi anaainisha matatizo
yanayotokana na uongozi mbaya unaofanywa na viongozi wabadhilifu na
wasiojali maslahi ya wengi, japo
wananchi waliwaamini kwa kuwapa fursa
hiyo kuongoza.Mwandishi amemaliza kwa kueleza kuwa
jamii mpya iliyokuwa na unyanyasaji, utabaka na vitu vingine visivyofaa
inawezekana pale watu wanapoamua kuungana na kufanya mambo kwa kuelewana na
ndio mwanzo hasa wa amani katika jamii. Tunayaona haya pale kichaa na mwanmke
walipoungana pamoja na kujenga jamii mpya isiyokuwa na ubaguzi, unyanyasaji na
utabaka. Kwa kifupi riwaya hii inadodosa maana ya maisha ambapo mwandishi
anasema maisha ni kama mkufu unaochukua kipande hiki na kile unaviunganisha,
kipande kimoja kikikatika unakiacha unachukua kingine kinachokufaa wewe hicho
kitamfaa mwingine, siku ya kufa kila mtu atavikwa mkufu wake.
Mwendo wa riwaya;
Hurejelea suala zima la kasi, mtiririko na mshindilio wa vitushi vya riwaya
kwa kuzingatia vigezo vya msuko, maudhui, masafa ya kiwakati na kijografia.
Mwendo wa riwaya hii ya “Mzingile” ni mwendo wa taratibu kutokana na kuwa na
maudhui yaliyojaa utanzia mwingi, masafa
ya kijiografia na yale ya kiwakati, yamebainishwa
wazi pia kunamshindilio mkubwa wa vitushi. Maudhui ya riwaya hii ni ya kitanzia.
Kwa mfano, msimulizi amekumbwa na matatizo na migogoro mbalimbali katika
harakati za safari zake za kumtafuta mzee. Msimuliaji anasema “Giza lilipoingia sikuweza kuziona nyayo
tena. Kwa kuogopa kupotea njia nilikata shauri kutafuta mahali pazuri pa
kulala. Nilivua shati nikafunikia uso wangu ili mchanga usiingie machoni
mwangu. Niliota. Niliota mtu akinisemesha. Mtu aliyekuwa akizungumza nami
alikuwa amefunikwa na hali ya mawingumawingu au labda ukungu. Sura yake
sikuweza kuitambua.Alinitazama bila kusema neno kwa muda. Nilijaribu kuinua
kichwa lakini kilikuwa kizito. Nilitaka kupiga kelele lakini kinywa kilikataa
kufunguka na ulimi ulikuwa mkavu” (uk 9-10)
Masafa ya kijiografia yamebainishwa wazi kama vile kijijini kwa mfano “Siku ambayo mama yake aliumwa uchungu,
aliitwa mkunga mashuhuri kijijini kuja kumhudumia” (uk1), msituni, kwa
mfano “Yasemekana Kakulu alipojiona mzee aliwateua wazee watano, mmoja kila
kijiji akaenda nao msituni” mlimani (uk 11).
Masafa ya kiwakati nayo pia yamebainishwa wazi ili kumpa msomaji nafasi ya
kujua kile msimuliaji amekikusudia kwa mfano mwandishi anasema “Ilikuwa jioni kama saa kumi nilipoamka.
Macho yalikuwa mazito. Katika jitihada ya kutaka kuona niliona mwanamke
amesimama karibu name akinitazama” (UK 9). Masafa ya kiwakati yameonekana
pia katika (uk 4, 13, 44).
Naratolojia;
Ni taaluma inayohusu suala la usimulizi katika kazi za
kiuandishi. Katika taaluma hii ya usimuliaji, kuna masuala mbalimbali
yanayojitokeza kama matumizi ya nafsi, suala la wakati na mwendo wa kazi
husika. Katika riwaya hii ya “Mzingile” mwandishi ametumia usimulizi shahidi na
usimulizi maizi.
Usimulizi shahidi umejitokeza ambapo pana matumizi ya nafsi ya kwanza.
Mfano, “Safari yangu ilianza asubuhi na mapema wakati ambapo fikra zilikuwa
bado kuchoka. Sikujua nielekee upande gani maana hakuna aliyejua kwa hakika
mahali alipoishi. Nilifuata silka zangu” (UK 7) pia usimulizi huu umeruhusu
kupenyeza matumizi ya nafsi ya pili, katika ukurasa wa pili kunamatumizi ya
nafsi ya pili kwa mfano,“Na ninyi mnatafuta umbea! Ondokeni hapa! ” (uk 2).
Usimulizi maizi pia umetumika pale mwandishi alipotumia nafsi ya tatu kwa
mfano “Wazee walikumbuka kuwa alipenda sana ubuyu, walianza kutoa sadaka
chini ya mibuyu….” (uk 4)
Mtagusano
Ni athari au mwingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi za fasihi, kwa
kawaida hii inahusishwa na mwigo au uathiriano wa kazi moja na nyingine.
Vipengele hivyo vyaweza kuwa usawiri wa wahusika, lugha, mandhari, na maudhui.
Vifuatavyo ni vipengele vya mtagusano kama
vilivyojitokeza katika Riwaya ya “Mzingilie”
Usawiri wa wahusika.
Usawiri wa wahusika, ni kitendo cha kuwachora, kuwafafanua, kuwatambulisha
na kuwajenga wahusika huku wakipewa maneno, matendo, hadhi na uwezo unaolandana
na unaowiana. Mwandishi amesawiri wahusika kwa namna ifuatayo;
Mbinu ya mtunzi kumwelezea mhusika, hii ni mbinu ambayo mtunzi huitumia
kumwelezea mhusika juu ya matendo yake, mienendo na tabia za mhusika. Kwa
mfano, katika riwaya ya “Mzingile” mtunzi amemwelezea Kakulu kama ifuatavyo; “Kakulu alitunza vizuri migomba iliyoachwa
na mama yake, alilima viazi na mahindi, akaishi kwa kujitegemea. Alizoea
kuwatembelea majirani zake asubuhi na mapema akimung’unya ubuyu…..”(UK 2).
Mbinu ya uzungumzaji nafsi, hii ni mbinu ambayo mhusika
huzungumza na nafsi yake mwenyewe. Katika riwaya hii ya “Mzingile” mbinu hii
imetumika pale Mhusika Kichaa anazungumza na nafsi yake “Ninataka kuwa kichaa!”. Kwa sauti yenye kutisha nilipiga kelele, “Ninaweza
kuuwa mtu nikamla mzimamzima!” (UK 20).
Mbinu ya kuzungumza na hadhira, mbinu hii inatumika ambapo
mwandishi humchora mhusika akizungumza na hadhira, hadhira huweza kumfahamu
mhusika kupitia mazungumzo yake mwandishi ametumia mbinu hii ambapo mhusika
Kakulu amezungumza na hadhira kwa mfano mwandishi anasema “…akawakaripia wanaume waliokuwa karibu, ondokeni hapa! Mnachuguliachungulia
nini? Hampashwi kuona mwanzo wangu na njia niliyoijia!” (uk 1) pia Kakulu
anazungumza na wanawake waliokuwa karibu naye “Na ninyi mnatafuta umbea! Ondokeni hapa! ” (UK 2)
Mbinu ya mhusika kuwafafanua wahusika wengine,
kwa mfano
sehemu ya sita mwandishi amewachora baadhi ya wahusika wakiwazungumzia wahusika
wenzao na matendo yao kwa mfano maongezi ya msimulizi na kijana, mfuga mijusi
“Ulimwona?”
“Nani?”
“Mzee”
“Unamjua!”
“Alipita hapa na blanketi lake
akiwa amejiharishia.
Amezeeka sana sasa.Alitembea kwa kuyumbayumba kama aliye ndotoni”. (Uk 56)
Mbinu ya majazi, hii ni mbinu ya kuwapa wahusika
majina kulingana na sifa zao, tabia au dhima anazotakiwa kupewa. Katika riwaya
ya “Mzigile” jina la mhusika Kakulu alipewa kulingna na sifa yake ya kuzaliwa
akiwa na uwezo wa kufanya matendo yanayopashwa kufanywa na watu wenye umri
mkubwa. Kwa mfano mwandishi anasimulia “Wanakijiji
walimpa jina la Kakulu kwa sababu alizaliwa akiwa na ndevu tayari-Kakulu,
kakubwa, kazee” (UK 1)
Mandhari
Mandhari iliyotumika ni kama vile; kijijini kwa mfano, “Siku ambayo mama yake aliumwa uchungu,
aliitwa mkunga mashuhuri kijijini kuja kumhudumia” (UK 1), mandhari ya
msituni uk 4 “Yasemekana Kakulu alipojiona mzee aliwateua wazee watano, mmoja
kila kijiji akaenda nao msituni” mlimani uk 11, majini uk, baharini uk…
Matumizi ya lugha
Ametumia
lugha ngumu iliyojaa picha Kwa mfano, ametumia
mizinga, nyuki na asali. Mzinga ni nchi, asali ni rasilimali na nyuki ni
wananchi (UK 77), kundi la mijsi kubadilika kuwa ng’ombe (UK 55) ni sawa na
viongozi wasiowaadilifu kujigeuza na kuonekana kama wanatenda wema kwa wananchi
wao, pia ametumia mbinu ya safari ndefu yenye mahangaiko kuwakilisha hali
halisi ya maisha ya binadamu na misukosuko waipatayo binadamu
Ametumia semi mbalimbali kama vile
methali na misemo kwa mfano
ametumia methali kama vile “Asiyesikia la mkuu
huvujika guu! Ulimwengu huu haukusikia la mkuu” (uk
2), ametumia pia misemo kama vile “mkubwa
haibi, anachukua” msanii anasema “Wazee wakaanza kugawana kile kidogo
kilichokuwepo. Msemo ukawa mkubwa haibi, anachukua” (uk2),
Ametumia tamathali za semi mbalimbali kama vile
sitiari, tashibiha, nk kwa mfano, ametumia tashibiha pale aliposema “Maisha ni
kama mkufu” (UK 7),”Hata hivyo watu walikufa kama panya” (UK 54),
Ametumia pia tashihisi pale mwandishi anasema
“Nitakupeleka,”pundamilia alisema (UK 83)
Maumizi ya mbinu nyingine za kisanaa kama vile;
nidaa (UK 23)
Matumizi ya Mbaalaga, kwa mfano mwandishi anasema
“Ikafikia hatua ya binadamu kumla binadamu mwenzake” (UK 54)
Matumizi ya kejeli, kwa mfano “Kawaimbieni nyimbo
hizo wake zenu” (UK 53)
Matumizi ya lugha changamani kwa mfano, ametumia
maneno ya lugha ya kiingereza kama vile, “Beyond reasonable doubt” (UK 41),
well done (UK 47), once more (UK 56)
Mianzo na miisho ya riwaya
Hii ni namna riwaya zinavyofunguliwa au kusanwa na
kumalizia. Riwaya inaweza kuanza na taharuki, maswali/kiu au wakati mwingine
simulizi. Riwaya ya “Mzingile” sehemu ya kwanza imeanza na simulizi juu ya
maisha ya Kakulu na kuzaliwa kwake kimaajabu. Kwa mfano msanii anasema
“WALIMWITA Kakulu. Sasa bado tunamwita Kakulu na wajao watamwita hivyohivyo.
Ukweli wake ulizingirwa na ukungu wa kisasili. Hakuna mtu aliyewajua barabara
wazazi wake. Kuwako kwake kulianza kama mzaha.yasemekana kuzaliwa kwake
kulikuwa kwa ajabu”(UK 1)
Riwaya hii pia imeishia na hali ya taharuki kwa
mfano………………………………………………..
Mtindo katika riwaya ya
Mzingile
Ameigawa kazi yake katika sehemu mbalimbali kama vile
sehemu ya kwanza (UK1-UK 5), sehemu ya pili(UK6-) sehemu ya tatu sehemu ya nne sehemu
ya tano sehemu ya sita sehemu ya saba
Matumizi
ya nyimbo kwa mfano katika ukurasa wa 33,na 78.
Ambapo kuna matumizi ya wimbo.
“Ninaimba juu ya giza
liligubika ulimwengu.
Tumetembea katika msitu wa kurasa potovu
Na kutafuna kila neon na kila aina ya wino.
Tumemeza yapashwayo kunywewa
Na kucheua yatakiwayo kumezwa.” (UK
33)
Pia ametumia muziki ili kuihaisha kazi yake kwa mfano uk 46 mwandishi
anasema “Saa mbili kamili mambo yalianza. Pazia tu lilipoinuliwa tu vifijo
vilianza kusikika sehemu ya nyuma. Muziki wa kuingilia uliwekwa. Msichana wa
kwanza aliinigia akicheza kwa mwendo wa haraka haraka uliodhihirisha uhai wake…”
UK
46
Matumizi ya dayolojia kwa mfano sehemu ya sita (uk 51) kuna mazungumzo ya
msimulizi na watoto waliokuwa wanawinda
“Mnakaa peke yenu?”
“Hapana. Yupo kaka”
Kijiji chenu kikubwa? Walitazamana na sikupata jibu
“Kuna kanisa? Niliendelea”
“Kaka ametukataza tusiseme mengi kwa wageni” (UK 51)
Matumizi ya barua kwa mfano (uk 64 na 65) mwandishi anasema , juu ya sehemu
hii nyeusi maandishi hafifu yaliweza kuonekana. Niliposogea karibu niliweza
kuyasoma: “Kwa mtakaosalia. Msifanye
makosa tuliyofanya sisi. Tulifunzwa hatukufunzika. Hatukuweza kuongoza mkondo
wa sayansi na uchumi, siasa iliposhika hatamu…….”(UK 64)
Matumizi ya nafsi zote tatu kwa mfano
Pia mwandishi amechanganya lugha ya kiswahili sanifu na maneno ya lugha za kikabila kama vile neno Kakulu pia
maneno ya lugha za kigeni kama vile kiingereza na kilatini kwa mfano, “ Beyond reasonable doubt” (UK 41), well done (UK 47), once more (UK 56)
UBUNILIZI KATIKA RIWAYA YA MZINGILE
Ubunilizi ni neno
linalotokana na neno buni lenye maana ya kutengeneza kitu kwa mara ya kwanza,
gundua, zua au tunga jambo (Kamusi ya Kiswahil Sanifu:34).Hivyo basi fasihi si
kazi inayohusu mambo ya kipekee bali ni uwasilishaji wa maisha ya jamii kwa njia
bunifu isiyo ya moja kwa moja. Mbinu za kibunilizi zilizotumika katika Riwaya
ya “Mzingile” ni kama zifuatazo;
Ufumbaji ni utumiaji wa kauli zenye maana fiche katika kazi ya fasihi. Kauli hizo
huwa na maana kinyume na kazi zinazohusika. Katika kazi za fasihi ufumbaji
hutumiwa kwa malengo tofautitofauti kama vile; kukwepa mkono wa dola, kuepuka
kugusa hisia za wahusika moja kwa moja na pia kuwapa wasomaji nafasi ya
kuwafikirisha. Katika riwaya hii ufumbaji umejitokeza katika sehemu mbalimbali.
Kwa mfano, ametumia mizinga nyuki na asali (UK 77). Mzinga ni nchi, asali ni
rasilimali na nyuki ni wananchi, kundi la mijsi kubadilika kuwa ng’ombe (UK55)
ni sawa na viongozi wasiowaadilifu kujigeuza na kuonekana kama wanatenda wema
kwa wananchi wao, pia ametumia mbinu ya safari ndefu yenye mahangaiko
kuwakilisha hali halisi ya maisha ya binadamu na misukosuko waipatayo binadamu
Usawiri wa wahusika, ni kitendo cha kuwachora,
kuwafafanua, kuwatambulisha na kuwajenga wahusika huku wakipewa maneno,
matendo, hadhi na uwezo unaolandana na unaowiana. Mwandishi amesawiri wahusika
kwa namna ifuatayo;
Mbinu ya mtunzi kumwelezea mhusika, hii ni mbinu ambayo mtunzi
huitumia kumwelezea mhusika juu ya matendo yake, mienendo na tabia za mhusika.
Kwa mfano, katika riwaya ya “Mzingile” mtunzi amemwelezea Kakulu kama
ifuatavyo; “…Kakulu alitunza vizuri
migomba iliyoachwa na mama yake, alilima viazi na mahindi, akaishi kwa
kujitegemea. Alizoea kuwatembelea majirani zake asubuhi na mapema akimung’unya
ubuyu…..”(UK 2).
Mbinu ya uzungumzaji nafsi, hii ni mbinu ambayo mhusika huzungumza na nafsi yake
mwenyewe. Katika riwaya hii ya “Mzingile” mbinu hii imetumika pale Mhusika
Kichaa anazungumza na nafsi yake “Ninataka
kuwa kichaa!”. Kwa sauti yenye kutisha nilipiga kelele, “Ninaweza kuuwa mtu
nikamla mzimamzima!” (UK 20).
Mbinu ya kuzungumza na hadhira, mbinu hii inatumika ambapo mwandishi
humchora mhusika akizungumza na hadhira, hadhira huweza kumfahamu mhusika
kupitia mazungumzo yake mwandishi ametumia mbinu hii ambapo mhusika Kakulu
amezungumza na hadhira kwa mfano mwandishi anasema “…akawakaripia wanaume waliokuwa karibu, ondokeni hapa! Mnachuguliachungulia
nini? Hampashwi kuona mwanzo wangu na njia niliyoijia!” (uk 1) pia Kakulu
anazungumza na wanawake waliokuwa karibu naye “Na ninyi mnatafuta umbea! Ondokeni hapa! ” (UK 2)
Mbinu ya mhusika kuwafafanua wahusika wengine, kwa mfano sehemu ya sita mwandishi
amewachora baadhi ya wahusika wakiwazungumzia wahusika wenzao na matendo yao
kwa mfano maongezi ya msimulizi na kijana, mfuga mijusi
“Ulimwona?”
“Nani?”
“Mzee”
“Unanjua!”
“Alipita hapa na blanketi lake
akiwa amejiharishia.
Amezeeka sana sasa.Alitembea kwa kuyumbayumba kama aliye ndotoni”. (Uk 56)
Mbinu ya majazi, hii ni mbinu ya kuwapa wahusika majina kulingana na sifa zao, tabia au
dhima anazotakiwa kupewa. Katika riwaya ya “Mzigile” jina la mhusika Kakulu
alipewa kulingna na sifa yake ya kuzaliwa akiwa na uwezo wa kufanya matendo
yanayopashwa kufanywa na watu wenye umri mkubwa. Kwa mfano mwandishi anasimulia
“Wanakijiji walimpa jina la Kakulu kwa
sababu alizaliwa akiwa na ndevu tayari-Kakulu, kakubwa, kazee” (UK 1)
Mbinu
ya utanzia, ni mbinu
ambayo mtunzi hutumia vipengele mbalimbali vizuavyo huzuni, jitimai,
masononeko, masikitiko na mateso kwa hadhira yake. Kipengele hiki ni kinyume na
ufutuhi, katika riwaya hii ya Mzingile mwandishi ametumia utanzia kama
ifuatavyo; mateso, kifungo, vifo, ugumu wa maisha, magonjwa njaa, ukame na mahangaiko
kwa ujumla. Kwa mfano, mwandishi anasimulia jinsi mwanamke wa kiafrika
alivyokamatwa, akafungwa jela, akauwawa na pia kunajisiwa. Msanii anasema “Walimfunga, wakampeleka chumbani kwa
meneja. Baada ya kumpiga viboko walimfungua. Alianza tena kupigana nao.
Walimuua akipigana. Walimnajisi huku akiwa amekufa” (Uk 50), ameongelea pia
suala la ukame uliosababisha watu, mimea wanyama na wadudu kufa na kupotea kwa
sababu ya ukame uliokikumba kijiji baada ya msimulizi kwenda safari ya
kumtafuta mzee msanii anasema “Ukame
ukaanza tena, ukaweka chachu ya dhuluma. Wao wakiuana, wanyonge wakifa njaa.
Ukame ukaongeza ukakasi. Vifo vikazidi kuongezeka” (uk 51-55).
Mbinu
ya ufutuhi, ni mbinu
ambayo msanii hutumia ucheshi au furaha kwa hadhira yake.Hii ni kinyume na
tanzia. Katika riwaya ya “Mzingile” mwandishi anaonesha ufutuhi pale
anaposimulia vituko vya Kakulu aliyekuwa na tabia ya kuwaingilia mapadri,
masisita, mashehe kwenye baibui na kanzu zao. Kwa mfano, msanii anasema “Alikuwa
mtani wa kila mtu. Mapadri wa siku hizo, masista, wavaa baibui na mashehe
walikaogopa, maana kalizoea kufunua makanzu yao na kuingia miguuni mwao. Ilikuwa vigumu
kukaondoa humo. Utawasikia wakipigapiga makanzu yao
kama kwamba wanatoa vumbi, We Kakulu acha
kufanya hivyo!”. Kalichowafanyia wao wenyewe walijua (UK 3) Pia wenye mabinti
walimtania Kakulu awapelekee maji na kuni ili wampatie binti wa kuoa, kwa mfano
masnii anasema “Kwa hiyo wenye mabinti wakawa wanakatania. Ukinitafutia kuni
nitakupa binti uoe. Jioni hiyo utamwona Kakulu anapeleka mzigo wa kuni
uliomzidi kimo” (uk 3) pia
Kakulu kumtia mimba mwari kimzaha (uk 3)
Mbinu
ya taharuki, taharuki ni
matarajio ambapo tunahamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye Wamitila (2003),
hivyo basi, ni hali ya kuwa na dukuduku la kutaka kujua juu ya nini kitafuatia
katika usimulizi wa kazi za fasihi, mtunzi huijengea hamu hadhira yake ya
kutaka kujua zaidi.Mbinu hii imeoneshwa katika’’ Riwaya ya “Mzingile” pale mwandishi amekatakata matukio kwa kurukia
tukio jingine kwa mfano tukio ……….., kaanza na tukio tokeo (uk 1) na baadae
tukio chanzi uk……, msanii ameanza kwa kusema “WALIMWITA Kakulu. Sasa bado
tunamwita Kakulu na wajao watamwita hivyohivyo.” Pia anwani yenyewe Mzingile
imejengwa kitaharuki kwani pale msomaji aonapo anwani hii atakuwa na shauku ya
kuisoma ili apate kujua maana halisi ya anwani hii.
Utomeleaji, ni kuingiza baadhi ya kaida za kazi fulani kwenye kazi nyingine.
Tunatomelea ili kuipa uhai kazi ya fasihi na kuifanya hadhira ijione kuwa ni
sehemu ya kazi hiyo au kazi husika. Katika riwaya hii ya Mzingile utomeleaji
umejitokeza katika ukurasa wa 33,na 78. Ambapo kuna matumizi ya wimbo.
“Ninaimba juu ya giza
liligubika ulimwengu.
Tumetembea katika msitu wa kurasa potovu
Na kutafuna kila neon na kila aina ya wino.
Tumemeza yapashwayo kunywewa
Na kucheua yatakiwayo kumezwa.” (UK
33)
Pia ametumia muziki ili kuihaisha kazi yake kwa mfano uk 46 mwandishi
anasema “Saa mbili kamili mambo yalianza. Pazia tu lilipoinuliwa tu vifijo
vilianza kusikika sehemu ya nyuma. Muziki wa kuingilia uliwekwa. Msichana wa
kwanza aliinigia akicheza kwa mwendo wa haraka haraka uliodhihirisha uhai wake…”
UK
46
Mbinu
ya ritifaa, ni mbinu
ambayo mtunzi huwasilisha mambo kwa kuwaonesha wahusika wake wakiwasiliana na
mtu aliyembali (umbali wa kijiografia au aliyefariki).mfano katika riwaya ya
Mzingile
mwandishi
amemuonesha …………………………………………………………….
Dayolojia, hii ni mbinu ya kutumia kauli za kiusemezano kwa lengo la kufikisha ujumbe
uliokusudiwa. Mtunzi hutumia vinywa vya wahusika ili kufikisha
ujumbe. Katika riwaya ya Mzingile mbinu hii imetumika kama
njia ya kuonyesha ufundi wa mtunzi kuweza kusawiri wahusika na hadhi zao pia
imesaidia kuwasilisha mawazo kwa hali ya uasilia kwa sababu wahusika wenyewe
wamwtamka maneno kwa vinywa vyao wenyewe. Katika riwaya ya Mzingile kuna
mazungumzo ya wahusika mbalimbali kwa mfano kuna mazungumzo kati ya msimulizi
ma mzee (uk 14)
“Nimetumwa kuja kukuona”
“Mimi”
“Ndio. Wewe”
“Kuhusu”
“Kifo cha mwanao. Nimekuja
kukujulisha kuwa mwanao ameuawa”
Mbinu ya ujadi, ni utumiaji wa kauli za asili, kauli
zinazofungamana sana
na jamii inayoandikiwa.Hutumika zaidi ili mwandishi aweze kujipambanua kuwa
naye ni sehemu ya jamii ile. Kauli hii hujumuisha methali, nahau, misemo na
vipengele vinginevyo vya kimazungumzo, mfano katika Riwaya ya Mzingile ametumia
methali kama vile “Asiyesikia la mkuu huvujika
guu! Ulimwengu huu haukusikia la mkuu” (uk
2), ametumia pia misemo kama vile “mkubwa
haibi, anachukua” msanii anasema “Wazee wakaanza kugawana kile kidogo
kilichokuwepo. Msemo ukawa mkubwa haibi, anachukua” (uk2), pia ametumia maneno
ya kijadi kama
vile jina la Kakulu ni la kijadi likiwa na maana ya kakubwa, kazee
kalikokomaa. Matumizi ya usihiri pia yandhihirisha ujadi katika jamii, kwa mfano tukio la mijusi
kugeuka kuwa ng’ombe (uk
55)
Hivyo basi
kupitia mbinu hii ya ujadi hadhira hujiona iko karibu sana na kazi husika
waonapo baadhi ya vipengele vya usimulizi wa kijadi wavitumiavyo katika jamii
zao vimetumika katika kazi husika
Mbinu
ya kisengerenyuma, ni
namna ya usimuliaji ambao huanza na tukio- tokeo kisha hufuatia tukiochanzi,
mbinu hii mtunzi huelezea kitu na baadae asili au mwanzo wa kitu kile.Mbinu hii
imeneshwa pia katika Riwaya ya “Mzingile ’’kuanzia (uk1) anazungumzia habari ya
Kakulu kuitwa Kakulu na watu wa kale, waliopo wanamwita kakulu na wajao pia
watamwita Kakulu. Kwa mfano mwandishi anasema “WALIMWITA Kakulu. Sasa bado
tunamwita Kakulu na wajao watamwita hivyihivyo.” Halafu baadae akasimulia kisa
cha Kakulu kuitwa Kakulu
Msuko
wa vitushi katika riwaya ya Mzingile
hiki ni
kipengele kingine kilichotumiwa na waandishi katika kuwapa wasomaji hamasa ya
kuendelea kusoma kazi ya fasihi unajumuisha mambo kama
vile muwala na motifu mbalimbali. Mfano, katika Riwaya ya Mzingile
Muwala
Katika
riwaya ya mzingile kuna mwendelezano wa vitushi katika kila sehemu, vitushi
hivyo vinajengana kiasi cha kuleta mwendelezo wa matukio katika usimulizi. Kwa
mfano katika sehemu ya pili kuna vitushi viwili, kitushi cha kwanza kinahusu
kifo kilichompelekea msimulizi kuanzisha safari ndefu ya kumtafuta mzee
aliyeishi sehemu za mbali, msimulizi anasema “Safari yangu ilianza asubuhi
na mapema wakati ambapo fikra zilikuwa bado kuchoka. Sikujua nielekee upande
gani mana hakuna aliyejua kwa hakika mahali alipoishi” (uk7) pia kisa cha
mzee kuishi mafichoni kimejitokeza katika sehemu hii ya pili (uk 16) kwa mfano
mwandishi anasimulia “Kwa kuwa nilikuwa na tuhuma ya kusalitiwa nilijenga
nyumba hii ili kujikinga na ghadhabu ya wale ambao wangependa kujilipiza kisasi
wakati nimeishiwa nguvu……..Ndiyo maana niko hapa mafichoni” (uk 16) Sehemu
ya saba inakamilisha safari yamsimulizi aliyekuwa anapeleka taarifa ya kifo kwa
Mzee.
Mtirirko
wa matukio au vitishi umeleta ujumbe unaoeleweka kwa wasomaji.
Motifu
Motifu
ya safari, mwandishi
ametumia motifu ya safari kuanziz sehemu ya pili mpaka sehemu ya saba. Kwa
mfano uk
7 msimulizi alianza safari ndefu ya kumtafutaKakulu msanii anasema “Safari
yangu ilianza asubuhi na mapema wakati ambapo fikra zilikuwa bado kuchoka.
Sikujua nielekee upande gani mana hakuna aliyejua kwa hakika mahali alipoishi”
(uk7)
Motifu
ya ndoto, mwandishi
ametumia motifu hii ya ndoto katika (uk
9-10) ambapo mwandishi anasema “Giza lilipoingia sikuweza kuziona nyayo tena.
Kwa kuogopa kupotea njia nilikata shauri kutafuta mahali pazuri pa kulala.
Nilivua shati nikafunikia uso wangu ili mchanga usiingie machoni mwangu.
Niliota. Niliota mtu akinisemesha. Mtu aliyekuwa akizungumza name alikuwa
amefunikwa na hali ya mawingumawingu au labda ukungu. Sura yake sikuweza
kuitambua.Alinitazama bila kusema neon kwa muda. Nilijaribu kuinua kichwa
lakini kilikuwa kizito. Nilitaka kupiga kelele lakini kinywa kilikataa
kufunguka na ulimi ulikuwa mkavu” (uk 9-10)
Motifu
ya majini, msanii
ametumia motifu hii katika (uk
8-11) kwa mfano msanii anasema “Nilipotoka majini nilijisugua mwili mzima
hadi mapafu yalipohitaji hewa tena. Nilijitubukiza tena majini, nikaondoa
uchafuuliokuwa umekokomolewa na mchanga” (uk 8)
MAREJELEO
Kezilahabi, E (2011), Mzingile, Toleo la tatu: Dar es
Salaam University Press: Dar es salaam
Tuki (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi:
Oxford University Press.
Wamitila, K. (2003); Kamusi
ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Focus Publications Ltd, Nairobi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni