Mafanikio ni juhudi binafsi.
Na
Gabriel Manoko
O712708790
Kuna wakati unakutana na
mtu anakusimulia historia ya maisha yake na mafanikio ambayo kayapata unabaki
umeduwaa, unaweza ukawa unashangaa lakini mwisho unaona manufaa ya kutumia
vizuri akili ambazo tumepewa na mwenyezi Mungu, kufikiria na kufanyia kazi
mambo yanayoweza kubadilisha maisha.
Kwangu huyu ninaweza kumuita msichana mwenye malengo ya mbali , ana
akili pia anatumia maamuzi sahihi na busara kwa kuamini kuwa uthubutu wa
kufanya jambo huleta mabadiliko makubwa ya maendeleo kwenye jamii na hata
kwenye familia yake.
Huyu si mwingine,
bali ni Suzana Raphael (22) msichana ambae kwa makala hii anaweza kuwa chachu
ya wasichana wengine wa hapa kwetu Tanzania na hata nje ya nchi kwa kuona
thamani ya kufanya swala zima la u modal na
kuweza kujipatia kipato halali na kuweza kujipanga kuondokana na umasikini.
Suzana ni modal ambaye
anafanya kazi na wanamitindo (Designers) mbalimbali kama Mustafa Hasanari na
Hadija Mwanamboka, ambapo aliweza kuonyesha mavazi mbalimbali katika show tofauti tofauti kama Swahili
fashion na Red in red ambazo zilifanyika mkoani Dar es salaam.
Historia ya elimu
Suzana ni mzaliwa wa
Musoma na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya watoto watatu, ambapo
aliweza kumaliza darasa la saba mwaka (2004), na kuweza kuendelea na elimu ya
kidato cha kwanza mwaka (2005). Na alimaliza
kidato cha nne mwaka (2008)katika shule ya Baptist Sekondari ambayo ipo
Magomeni Mkoani Dar es Salaam.
Kuingia kwenye Umodal wa mavazi
“Baada ya kumaliza
kidato cha nne kipindi kipindi yupo kidato cha pili katika shule ya sekondali
ya Perfect Vision aliweza kushiriki mashindano mbalimbali ambayo yameandaliwa
na shule ,”anasema.
Lengo la mashindano
hayo ilikuwa ni kuwakalibisha wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo
ya Perfect Vision,” anasimulia Suzana
Kuna siku alikutana na Nancy Sumari maeneo ya Ubungo na ndipo aliambiwa
na Nancy kuna shindano la Kisura ambalo linazaminiwa na Psi na usaili
utafanyika Club Maisha ambayo ipo Dar es salaam maeneo ya Osterbay. Alifika
kwenye ukumbi huo na aliweza kukutana na wadada wengi ambao walikuwa wanasubiri
usahili na yeye alifanikiwa kushinda na kwenda kambini kwa ajili ya mashindano
hayo. Waliweza kukaa kwenye hoteli ya Kiromo ambayo ipo Bagamoyo na waliweza
kukaa huko kwa muda wa miezi mitano,” anasema Suzana
Aliweza kuingia kwenye fainali ya mashindano hayo ambayo yalifanyika
katika hoteli ya Serena hiliyopo Dar es salaam, mshindi wa kwanza alikuwa Eliza
na yeye alikuwa mshindi wa tatu na kuweza kupata msaada wa kwenda kusoma katika
chuo cha urembo kinachoitwa PURE na kutokana na mashindano hayo ndipo
wanamitindo (Designers) wakubwa wa hapa nchini kama Mustafa Hasanari na Hadija
Mwanamboka waliweza kumuona siku ya
fainali na kuanza kufanya nae kazi ya Umodal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni