Madumulla (2009) anasema,
riwaya ni nathari bunifu simulizi kama vile hadithi, hekaya na ngano
inayosimuliwa kwa mdomo.Anaendelea kusema kuwa fasihi ilitokana na maandiko ya
fani ya ushairi hususani tendi za kiswahili katika hati za kiarabu kwasababu
ndio maandishi yaliyotamba katika pwani ya Afrika mashariki.
Pia,
Muhando.P na Balisidya(1976)wasema, riwaya yaweza kuanzia maneno 35,000 na
kuendelea, lakini tukisema juu ya urefu na kuishia hapo tu,jambo hili halitakuwa
na maana. Maana mtu yeyote anaweza kuweka habari yoyote ile katika wingi wa
maneno kama hayo.Jambo muhimu hapo ni kuwa riwaya huwa na mchangamano wa
matukio,ujenzi wa wahusika, dhamira,muundo wake na hata mtindo.Mwandishi tuseme
ana uwezo wa kutamba na kutambaa mahali pengi na kutambaa vizingiti kama
apendavyo ili kujenga hadithi hiyo ndefu.
Vilevile,Wamitila (2003) anasema, riwaya ni
kazi ya kinathari au kibunilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha, msuko
uliojengeka vizuri,wahusika wengi walioendelezwa kwa kina wenye kuchukua muda
mwingi katika maandalizi na kuhusisha mandhari maalum.
Sanjari
na hao, Nkwera (1978) anasema, riwaya ni hadithi iliyo ndefu kuweza kutosha
kufanya kitabu au zaidi. Ni hadithi ya kubuniwa iliyojengwa juu ya tukio la
kihistoria au kuandikwa kwa mtindo wa ushairi au mfululizo wa kinaganaga katika
uelezaji wa maisha ya mtu au watu na hata taifa.
Kwahiyo,
tunaweza kusema kuwa riwaya ni kazi iliyoandikwa kwa mtindo wa kinathari ambayo
ina urefu wa kiasi fulani,ni pana, ina uchangamano wa kimtindo na kidhamira na
ina shughulikia masuala kadhaa katika mtazamo mpana wa wakati.Baaba ya
kuangalia maana ya riwaya kutoka kwa waandishi mbalimbali zifuatazo ni sifa za
riwaya kutoka kwa Madumila (2009) kama ifuatavyo;
Kwanza,
huwa na urefu na upana wa kutosha, maranyingi huusisha upana wa kijografia
inaweza kuchukua hata ulimwengu mzima. Kulingana na hali hiyo pia hufanya
kupatikana dhamira nyingi sana kwa sababu huhusisha mambo mengi kijiografia.
Pili,
riwaya haifungwi na sheria wala kanuni, utanzu huu huwa haufingwi na kanuni za
uandishi kama tanzu zingine kama ushairi. Maranyingi utanzu wa ushairi huwa
unakanuni zake za uandishi kama kufuata uandishi wa urari wa vina na mizani na
lugha ya mkato.
Tatu,
riwaya inauhitaji wa kusoma na kuandika, stadi hizi mbili huwa ni nguzo muhimu
katika utanzu wa riwaya. Kwa hiyo riwaya haina nafasi kwa jamii ambayo haijui
kusoma wala kuandika. Kwa hali hii utanzu kama ushairi inaweza kushughulikiwa
hata na mtu ambaye hana taaluma ya kusoma na kuandika mfano, Haji Gora Haji ni
mtaalamu wa mashairi lakini hana stadi za kusoma na kuandika.
Nne,
riwaya huitaji uchumi madhubuti kwa sababu huiitaji viwanda kwa ajili ya
kuchapa vitabu ili iwafikie walengwa. Kwa sababu riwaya huwa inaweza kuzungumzia
mambo mengi katika ulimwengu mfano ubepari, utandawazi na ujasusi.
Baada
ya kuangalia maana za riwaya na sifa mbalimbali za riwaya ifuatayo ni historia
ya mtunzi na utunzi wake kwa mujibu wa Swahili foramu;
Kyllo
W. W. alizaliwa mwaka 1966 mjini Machakos nchini Kenya ni mwandishi anayeandika
katika tanzu za ushairi, tamthilia, hadithi fupi na riwaya. Pia ameandika
vitabu kadhaa vya watoto. Hadi leo hii amechapisha riwaya tatu ambazo niNguvuyaSala (1999), Bina – Adamu! (2002) na Musaleo (2005). Riwaya hizi zilikuwa na
ubunifu sana wa kisanaa hadi zikafikia hatua za kushinda tunzo ya fasihi ya Jomo
Kenyatta mnamo mwaka 2001 na 2005. Pia
ni mhakiki wa fasihi ambaye amechapisha makala mbalimbali katika majarida ya
kiusomi Afrika, Ulaya na Marekani. Mwandishi ana shahada ya uzamifu(Phd) katika fasihi. Mwandishi huyu pia ameweza
kutunga vitabu vingine kama vile; Wingulakupita
(Tamthilia), kamusiyaMethali, kamusiyaMisemo na Nahaunauhakikiwafasihi. Mwandishi anasema alitumia mwaka mmoja kuiandika
riwaya ya Bina –Adamu. Kwa sasa Wamitila ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha
Nairobi.
Bina – Adamu!
ni riwaya iliyotumia sitiari ya kijiji kuangalia hali ya mataifa ya ulimwengu
katika kipindi hiki ambapo hali za kijamii, kisiasa na kiuchumi zinadhibitiwa
na ubepari wa mataifa yaliyoendelea. Hii niriwaya ambayo inaelezea mambo
mbalimbali ambayo yanaendelea kutendwa na mataifa yalioendelea dhidi ya mataifa
yanayoendelea yaliyo katika bara la Afrika. Riwaya ya Bina – Adamu! inaelezea mambo mbalimbali kama athari za ubepari
kama vile, Afrika na uongozi wa mabavu. Mwandishi wa riwaya hii aliamua kutunga
kazi hii ili kukemea utawala wa kibepari unaoendeshwa hadi leo hii na yanchi
Marekani kwa mataifa yanayoendelea.Baada ya kuangalia historia ya mwandishi na
utunzi wake ufuatayo ni uainishaji wa aina ya riwaya;
Kuna ainakuumbilizariwaya ambazoniriwayadhatinariwayapendwa.
Riwayahiiinaingiakatikaainayariwayadhati. Riwaya dhati ni riwaya zinazo jadili
mambo nyeti yanayo tokea katika jamii. Hutumia lugha nyoofu na fasaha, hivyo
riwaya hizi hazitumii lugha ya matusi. Riwaya
pendwa ni riwaya ambazo zinajadili masuala kama vile upelelezi, mapenzi,
ujasusi na ujambazi. Katika riwaya pendwa fani huchomoza zaidi kuliko maudhui.
Kwa kuzingatia kigezo cha fani, RiwayayaBina – Adamu!niriwaya changamani kwani,riwayachangamaniniriwayaambayohuhitajikusomwakwa
makini ili msomaji aweze kuelewa. Aghalabuhuwanamaudhuimenginawahusikawengiambaowanachangiakatikakujengawazokuu
la riwaya hii. Hiinikwamujibu wa www.gafkosoft.com/swa/riwaya
2009-2014.
Piasifazariwayachangamanizimetufanyakusemariwayahiinichangamanikwaniriwaya
changamanimaudhuiyakeyanatakiwakutafakarizaidiilikupatakilekilichokusudiwa.
Lichayasifahiyo, riwayachangamanihutumialughayamafumbozaidi.Sifahizizimeonekanakwakiasikikubwakatikariwayahii,
nasifahizondizozikafanyatuiwekekatikakundi la riwayachangamani.
Kwakuthibitisha
haya,mwandishiametumialughayamafumbokwakiasikikubwakatikakaziyake.
Kwanihajatajamojakwamojahadhira yake anayoiandikialakinikwakupitia mafumbonataswirazilizotumikaunawezakubashirimaeneonamazingirayanayozungumziwakatikariwayahii.
Mfano(uk.100), mwandishiametumialughayamafumbokuwarejeleawazeewalivyopambanakatikakipindi
cha harakatizaukombozi.Mwandishianasema,
“Wazeewalinielezamatatizomengiwaliyokabiliananayozamaniwalipokuwa
wakipambananamazimwiyaliyoivamianyumbamiakamingiiliyopita.”
Mwandishiametumiapichayamazimwikurejeleawakolonina
nchizakiafrikazilizovamiwakatikakipindi cha utawalawakikoloni.
Piakatikakuendeleakuthibitishakuwahiiniriwayachangamani
mtunzi ametumiataharukikatikauelezeajiwamatukio,hii ni kuwafanyahadhira wake
waendeleekuisomailikujuaninialikuwaamelengakuwasilishakwahadhira. Imejitokezakatikasuraya
kwanza yariwayaambapo msomajiakisomasuramojahataelewaninimwandishiamelengakuelezeaisipokuwahadimsomajiaendeleekusomasurazingineilikuunganishamatukionakupatamadhui
hii.
Baada
ya kujadili uainishaji wa riwaya zifuatazo ni dhamira chomozizilizojadiliwa na
mwandishi katika riwaya ya Bina – Adamu!;
Utabaka,
ni hali ya kuwepo na tofauti za kimaisha miongoni mwa wanajamii. Tofauti hizo
zinaweza kuwa za kiuchumi, kisiasa na kadharika. Katika riwaya ya Bina - Adamu! mwandishi ameonyesha
matabaka ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayojitokeza katika jamii.Mfano,
katika (uk. 67) mwandishi anasema,
“Nyumba nyingi zimeinamiwa na miti
mbalimbali ya matunda; miembe, mipapai,
michungwa, mikakao, mipira, minazi… Kila kiongozi amekaa huko juu paani,
huko ndiko anakochumia matunda kwa rahisi na kuwatupia watu walioko chini ambao
wameshikia ngazi ya kupanda juu. Lakini kuna wengine ambao wanachofanya ni kula
wakashiba kwanza kisha kuyatupa makaka, makokwa na maganda huko chini
yanakogang’ang’aniwa na umati mkubwa ulioko huko.”
Hapa
mwandishi anazisawili nchi nyingi za Afrika kwakuonyesa matabaka ya kisiasa
yaliyopo kati ya jamii na viongozi wao. Viongozi wengi wa Afrika hula na
kushiba ndipo huwakumbuka wananchi wake ambao ndiyo wameshikilia ngazi hiyo
ambayo wamepanda.
Mwandishi
anazidi kuonyesha utabaka wa kisiasa katika jamii ambapo viongozi ambao ndiyo
wameshikilia madaraka jinsi wanavyohamishamalighafi za wanajamii na kuzihamishia
nje ya nchi kwa manufaa yao binafsi. Anasema katika (uk. 67),
“Wengine wanaiba na kuhamishia
kwingine, labda ughaibuni.”
Pia
mwandishi anazidi kuonyesha matabaka yanayotokea katika jamii, kuna tabaka la
juu tabaka la kati na tabaka la chini. Tabaka la juu linaposhiba huwarushia
tabaka la kati, na tabakala katilinaposhiba hurushia tabaka la chini ambalo ni
wananchi. Mwandishi anaonyesha katika (uk. 69) anaposema,
“Nilimwangalia yule mtu aliyeketi
jukwaani. Ni kweli alikuwa akila matunda aliyokuwa akitunda kwenda kwenye mti
uliokuwa umeiinamia nyumba hiyo. Mengine aliyatupia jamaa waliokuwa kwenye
sehemu ya chini karibu na ukingo wa ngazi ya kupandia paani. Wasiyoyataka
waliyatupia nyuma yakaangukia umati mkubwa ulikuwa huko chini. Umati mwenyewe
umekodoa macho pima huko juu kama kuu anayemwangalia mwewe.”
Vilevile,
mwandishi ameonyesha matabaka ya kiuchumi katika riwaya ya Bina-Adamu!,ambapo jinsi viongozi wa ngazi za juu wanavyofuja pesa
za umma na kuwaacha viongozi wa ngazi ya chini na hata wananchi wakiwa na hali
mbaya ya kiuchumi. Hii imejidhihirisha katika (uk. 111) anasema,
“… Nilikumbuka kisa kilichotokea
siku fulani katika nchi yangu. Kuna wakati serikali ilipofuja pesa kununua
magari mengi ajabu kwa kuwa kulikuwa na mkutano fulani wa viongozi wa nchi huru
barani. Baada ya mkutanohuo, magari hayo yalipewa marafiki wa viongozi. Siwezi
kusahau hili kwa kuwa siku hizo, tulikuwa tukisoma na mkaguzi wa elimu wa wilaya
alikuwa akitembelea shule za kwetu kwa baiskeli.”
Mapambano
dhidi ya ukoloni, huonyesha jinsi jamii ilivyopambana dhidi ya ukoloni ili
kijikomboa na kupata uhuru. Katika riwaya ya Bina-Adamu mwandishi ameonyesha jinsi wazee walivyopambana katika
kuuondoa ukoloni. Hii inajitokeza katika (uk. 100) anasema,
“Wazee walinieleza matatizo mengi
waliyokabiliana nayo zamani walipokuwa wanapambana na mazimwi yaliyovamia
nyumba miaka mingi iliytopita,“Ilitubidi kuzitumia ala zozote tulizokuwa nazo;
majembe, miundu, hanjari, mishale, na kila kitu tuseme. Lakini hatimaye tulifanikiwa,
alieleza mzee mmoja usiku tukifurahia mbalamwezi”
Mwandishi
ametumia lugha ya picha ya Mazimwi akimanisha ‘Wakoloni’. Dhamira hii inasawiri nchi za Afrika zilizokuwa
zimetawaliwa na wakoloni na jinsi walivyopigana hadi kupata uhuru wao.
Historia
na uhistoria, dhamira za kihistoria zinalenga kuelezea mapito ambayo watu
wamepitia. Mfano; kabla ya ukoloni, harakati za ukombozi na hata baada ya
uhuru. Kabla ya ukombozi kazi nyingi zililenga kuwahimiza watu wajikomboe kwa
kueleza mabaya yaliyofanywa na wakoloni na baada ya uhuru zilihimizakujenga
jamii mpya. Dhamira hii ya historia na uhistoria imejitokeza katika riwaya hii
ya Bina – Adamu ambapo, mwandishi
anaelezea jinsi jamii zilivyopambana na ukoloni mpaka kuwaondoa wakoloni na
hatimaye kupata uhuru. Mwandishi anazidi kuelezea jinsi viongozi walioaminiwa
na kuchaguliwa kuingia kwenye utawala baada ya ukoloni jinsi walivyowasaliti
wananchi. Anasema katika uk. 100
“Wazee walinieleza matatizo mengi waliyokabiliana
nayo zamani walipokuwa wanapambana na mazimwi yaliyovamia nyumba miaka mingi
iliytopita”.
“Ilitubidi kuzitumia ala zozote
tulizokuwa nazo; majembe, miundu, hanjari, mishale, na kila kiyu tuseme. Lakini
hatimaye tulifanikiwa,” alieleza mzee mmoja mmoja usiku tukifurahia mbalamwezi.
“Hatimaye tulifanikiwa kisha kikaja
kipindi cha ahadi za wenzetu waliokuwa na nguvu
za kuuongoza ukoo, tukawaamini. Kumbe
ni kosa kubwa tulilolifanya.” Walieleza
matatizo waliyoyapata siku hizi;
Karo ya watoto, upungufu wa chakula, magonjwa,
matatizo ya kazi….”
Hii
dhamira ya historia na uhistoria inasawiri nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania
kabla na baada ya uhuru. Lengo la mwandishi ni kuwaamsha watu ili waweze
kujenga jamii mpya ambayo haina matatizo kama hayo.
Utu
na maadili, dhamira hii ni pana kwani wapo wanaojadili maadili katika wigo wa
kisiasa na kidini dhamira ya utu na maadili huusisha vitu kama uchoyo, wizi, na
ubinafsi. Katika riwaya ya Bina–Adamumwandishi ameonyesha kuwa baadhi ya
viongozi hawana maadili ya uongozi kama mwandishi anavyosema (uk. 91),
“… mamanchi alipomuuliza akambaka
na kumuua. Ndugu yetu kabisa. Kakwea juu matunda anakula yeye tu na wenzake
wachache, wezi wote! Wanaiba hata mbegu …”
Mwandishi
anaonyesha jinsi viongozi wanavyoiba rasilimali za nchi bila kubakiza kitu.
Vilevile mwandishi ameonyesha jinsi watalii (wageni) wanavyoharibu maadili ya
jamii husika pale wanapokwenda kinyume na mila na desturi za jamii husika
mwandishi ameyaonyesha haya katika (uk. 109) anaposema,
“… sikuwa na hakika kama alikuwa
akinicheka mimi au akimcheka mtalii aliyekuwa amevua maguo yake na aliyekuwa
akikimbia mbele za wenzake huku tumbo lake kubwa ajabu likichezacheza kama
dodoki.”
Dhamira
hii ikilinganishwa na maadili ya jamii za waafrika hususani Tanzania inaonyesha
kuwa mtu huyo hakuwa na maadili katika muktadha wa jamii husika (watanzania)
kwani kutembea tumbo nje nikinyume cha mila na desturi za watanzania.
Uongozi na uwajibikaji, kuna viongozi ambao
hawawasaidii wananchi wake kwa matatizo yanayotokea katika jamii. Viongozi
kwenda kinyume na matakwa ya wananchi wao kwa kukiuka ahadi walizoziweka kwa
wananchi wao, mfano katika (uk. 144) anasema,
“Nilikumbuka wanasiasa wa kwetu
ambao hawachukui hatua yoyote au kufanya jambo bilaKukumbushwa.”
Viongozi wengi katika jamii wakiona matatizo
hawachukui hatua ya kuyatatua mpaka maafa na matatizo makubwa
yanapotokea.Vilevile viongozi wengi wanatumia pesa za umma vibaya kwani
wanafuja mali bila sababu ya msingi. Badala ya kutumia katika kuleta vitu vya
maendeleo, vilevile hutumia pesa nyingi sana kwa kufanyia vitu visivyokuwa na
maendeleo katika jamii mfano katika (uk. 111) tunaona viongozi wanavyofuja mali
ya serikali bila msingi,anasema,
“nilikumbuka kisa kilichotokea siku
fulani katika nchi yangu,kuna wakati serikali ilipofuja pesa kununua magari
mengi ajabu kwa kuwa kulikua na mkutano fulani wa viongozi wa nchi huru barani.
Baada ya mkutano huo,magari hayo yalipewa marafiki wa viongozi. Siwezi kusahau
hili kwa kuwa siku hizo tulikua tukisoma na mkaguzi wa elimu wa Wilaya alikua
akitembelea shule za kwetu kwa baiskeli.”
Vilevile
viongozi wanatoa ahadi za uongo na kuwasaliti wananchi, katika (uk. 136) mwandishi
anasema,
“Tulipopata
uhuru tuliahidiwa kupata mashamba yaliyokua yamemilikiwa na
wenzangu.Uhuru
ulikuja,lakini tuliendelea kulima vikataa vyetu visivyokua na
rutuba.Viongozi
ndio wanayolima hayo mashamba.”
Dhamira
hii inasawiri maisha ya waafrika kwani viongozi wengi ni wasaliti,wanafujaji
pesa za umma kwakufanya kumbukizi kwa kutumia gharama kubwa,badala yakufanya mambo ya
kimaendeleo. Pia viongozi hawana utayari wa kutatua matatizo ya wananchi, mfano
mzuri nchi ya Kenya kuna sikukuu za
kumbukizi kama Jomo Kenyatta na Tanzania siku ya Mwalimu Nyerere, Karume na
sikukuu ya Muungano hadi kufikia hatua ya kutokutoa pesa za mikopo ya Elimu ya
juu na mishahara kwa watumishi wa umma kama Walimu na Maaskari.
Ukoloni
mamboleo,ni hali ya taifa moja kutawala taifa lingine kiuchumi,kifikra na
kiutamaduni. Mataifa yaliyoendelea hutawala mataifa yanayoendelea kama
Tanzania, Kenya, Uganda na Ruwanda katika nyanja zote hizo, mfano katika (uk.88)
mwandishi ameonyesha ubaya wa wawekezaji kwa kusema;
“…wamemwaga mafuta hapa samaki wafe wapate sababu ya kutuletea makopo.
Huku
juuwanatupa mabaki ya nyuklia.”
Hapa
tunaona kuwa mataifa yaliyoendelea wanavyoharibu malighafi za mataifa
yanayoendelea ili wapate kuongeza soko kwa kuuza bidhaa zao. Vilevilemwandishi
anaonyesha jinsi nchi za mataifa yaliyoendeleawanavyowafanyia majaribio ya
kisayansi katika nchi zinazoendelea kama za kiafrika (uk.125),
“wali..ge..uzwa…vitu
vya kufanyia..majaribio”
…”ya
nini”Niliuliza kwa mshangao mkubwa.
“kua…ngali…a…a..ma..t.oke…o
ya kaswende…katika mi..ili ya bin Adam.”
Vilevile
mwandishi anaendelea kuonyesha jinsi ukoloni mamboleo ulivyoshamiri katika nchi
za kiafrika, mfano katika (uk. 86) anaonyesha jinsi kituo cha elimu
kilivyofungwa baada ya amrikutolewa na nchi zilizoendelea.
“kilikua
kituo cha usomi hiki lakini alisema kifungwe.
“ Nani?”
…hawakutaka
kiendelee na utafiti wake wa kuifunua historia kwa kila mtu…”
Hapa
tunaona kuwa mataifa yaliyoendelea hawataki nchi zilizokua chini yao waweze
kujitambua kwani wanaweza kujikomboa
kutoka katika ukoloni mamboleo. Ukoloni mamboleo ni dhamira inayosawiri maisha
halisi ya nchi za kiafrika kwani ukoloni umeshamiri sana nchi za kiafrika. Kwamfano,
nchini Tanzania watoto wa shule za msingi hupewa chanjo kila mara na kusemekana
kuwa ni majaribio ya kutibu ugonjwa fulani.
Athari za utandawazi,utandawazi ni hali ya
dunia kuonekana kama kijiji kimoja, kunakua na uhuru wa watu kusafiri kutoka sehemu
moja na nyingine duniani, pamoja na uhuru wa kufanya biashara. Mwandishiameonesha
athari za utandawazikama ifuatavyo;kwanza mipaka kufutwa na tamaduni za dunia
kuingiliana, mfano katika (uk. 140) inaonesha,
“mipaka mingi imefutwa,tamaduni sasa zinaingiliana na sisi
tumewatangulia wengi
kwauchunguzi hata kuliko wenyewe.!”
Pili
ni soko huria, utandawazi unasababisha soko huria duniani yaani taifa lolote
duniani kuwa na uhuru wa kuuza na kununua bidhaa yoyote duniani,na madhara yake
mataifa yaliyoendelea kukua kiuchumi kwa kuwa na soko kubwa nchi nyingine, mfano
(uk. 146) anasema,
“kwani….haowanafanya
shughuli zao ni nani?
“wanasafirisha dhana za vita kwenda kuuza.”
“wanawauzia nani?”
“sijui
lakini nasikia kuna familia kadhaa wanagombana na hawa wanaamini karibuni
wanawanapigana.Wanataka kuliwahi soko.”
Hii
inasawiri maisha ya Afrika kwani nchi nyingi za Afrika wanauziwa bidhaa za vita
hata kama hamna vita.
Ubinafsishaji ni
dhamiranyingineambayoimejitokeza katika riwaya hii ya Bina- Adamu. Mwandishiameonyeshajinsiwananchi ambavyohawarusiwi
kutumia vitu vyao kwakuwa sharia haziwaruhusukwanitayariviwandahivyovimeshabinafsishwa.
Mfano, (uk. 5)
“Kunaninihapa ?”
“ Hikinikiwanda”
“ Chanini?”
“ Reconditioned cars”
“ Mnazitumia?”
“ Ahh, dekimasen?
Haiwezekani asilani.Sheriazetuzinakataza
Matumiziyamagarihayo!”
Piakatikaukurasahuuunaonyeshajinsiubinafsishajiunavyofanyakazinakusababishawatukukatazwakufanya
shughuliambazonihakiyaonahatawabinafsishaji wakajionawaondiowakuukwaniwanadirikihatakusemakamatutakataakubinafsishwa,
baadhiyamisaadaitasitishwa. Hiiimethibitishwanamwandishi aliposema,
“Karibuni tutaanza kuwauzia samaki
wabichi”
“Hawana samaki huko?”
“Wanao lakini hawana idhini ya
kuwavua, sisi tunayo,
wanapatikana kwenye maji ya
kimataifa; International
waters. Tuna wavua na kuwapakia
kwenye makopo huko huko
majini. Wanawapenda sana hawa wa
makopo. Kwao ndiyo
maendeleo hayo! Wakiyagomea na si
misaada ya kiuchumi kwao
tunaizuia.”
Pia
suala la ushirikiano, mwandishi amelionyesha kwa kutumia mhusika Mimi kurejelea
mambo ambayo walikuwa wakiyatenda enzi za utoto. Hii inamaanisha kabla ya
utandawazi kuingia katika nchi zetu. Mwandishi katika (uk. 57) anasema,
“Siku hizo tulikuwa tukienda kufuga
mifugo ya kijiji pamoja.
Hapakuwa na tofauti wala
hatukuwazia wapi ni wapi,
Tuliwalishapamoja… na kumbuka kuwa
hata siku hizo aliyekosa
miongoni mwetu aliweza kuadhibiwa
na mzazi yeyote sio lazima
awe wake. Lakini mambo yalikuwa
yamebadilika.”
Mwandishi
ameyaonyesha hayo ili kuonyesha jamii jinsi ilivyoathiriwa na utandawazi na
kuwafanya watoto wengi kuwa na viburi kwa watu wengine.
Kwa
mujibu wa Florence L. V. (2013) anasema, matukio ya ajabuajabu (usihiri) ni natukio
ya kiajabu ambayo si ya kawaida iwapo tutayaweka katika ulimwengu wa
kawaida.Haya ni matukio ambayo ni kinyume na matukio ya kawaida yanayotarajiwa
na binadamu wa kawaida.
Sifa
za uhalisia ajabu, au matukio ya ajabu ajabu (usihiri) katika riwaya ya Bina – Adamu ni kama zifuatazo;
Kwanza,
kuwepo kwa wahusika ambao si wakawaida. Katika riwaya ya Bina – Adamu kuna wahusika wa aina mbili, wahusika binadamu na
wasio binadamu. Mfano wa wahusika ambao ni binadamu ni pamoja na mhusikaMimi, P.P, Mwanamke, Wanaume, Babu …
wahusika ambao si binadamu ni pamoja na mhusika Joka, matendo yaliyowasilishwa na viumbe pamoja binadamu ambayo si
matendo ya kawaida ndio hudhihirisha uwepo wa usihiri katika riwaya hii kwa
mfano (uk. 19-20) mwandishi anaposema,
“… niliangalia lile joka huku
nikirudi nyuma nyuma huku sauti imenikwama. Kwenye mgongo wake kulikuwa na
maandishi: Vitas; labda hakuwa nyoka bali macho yalinicheza tu. Ghafla nilimwona akinyionyirika haraka
haraka nami nikarudi nyuma wanguwangu. Nilikanyaga sehemu laini iliyomeguka na
kunitupa chini. Lazima lile joka lilifuatia.”
Vile
vile mwandisha ametumia mhusika beberu katika kuwasilisha matendo ya ajabu katika
(uk. 14) mhusika Mimi anasema,
“Nilikaribia lakini nikalazimika
kurudi nyuma baada ya kuinusa harufu mbaya kama ya beberu. Lazima jitu hilo
lilitambua na kijiegeza nyuma. Beberu! Beberu! Beberu! Nilijianbia akilini
nikiliangalia beberu beberu beberu, linanuka beberuu!..Lilitoweka ghafla kisha
kikafuatia kicheko kikubwa.’’
Pili,
kuwa na matukio ya kiajabu. Ni matukio ambayo yapo tofauti na maisha halisi kwa
mfano, mtu kutembeajuu ya maji bila kuzama ni tukio la kiajabu. Mwandishi
amemuonyesha mhusika Mimi kutembea
juu ya maji katika (uk. 15) kama mwandishi anaposema,
“… hatukwenda sana kabla ya kutumbukia kwenye mto uliokuwa na maji mengi
ajabu. Lakini hatukuzama badala yake tulielea juu juu. Mwenzangu alinishikilia
na kwa kiasi fulani nikajihisi kama Petro aliyetembea juu ya maji.”
Tatu,
kuwepo hali za kushangaza na za kuogofya. Katika riwaya hii ya Bina - Adamu, hali ya kushngaza na
kuogofya imejitokeza katika (uk. 22) mhusika “Mimi” anasema,
“Niliangalia mikono yangu. Ilikuwa
ya mtu mzima, lakini vyanda vyake vilikuwa vya mtoto. Nilipigwa na mshangao
mkubwa lakini nikagutuka kuwa nilipokuwa nikiishi kwa babu nilikuwa mtoto.
Labda nilishaanza kukua lakini kwanini vyanda vyangu vilibakia kuwa vya mtoto
mdogo?”
Hali hii ya mtu mzima kurudi ni hali ya
kushangaza na kuogofya. Vilevile mwandishi ametumia matukio ya ajabu kwa
kuonyesha chakula na kinywaji kisichokwisha na chenye kushibisha mara moja. Katika
(uk. 134) mwandishi anasema,
“nilichukua kile kibuyu changu na
kukifungua kisha nikamnyooshea. Alikichukua bila ya kuuliza lolote
akayapigamafunda kadhaa na kuyameza kwa sauti iliyoweza kusikika na hata mtu
akiwa mbali.”
Baada
ya kufafanua maana ya riwaya, dhamira chomozi zilizojitokeza katika riwaya ya Bina –Adamu, riwaya inayofanana na
riwaya hii kimaudhui ni Mzingile
ufuatao ni ufanano wa riwaya hizi kimaudhui.
Matabaka na utabaka. Suala la matabaka
limeweza kujadiliwa kwa kina sana katika riwaya ya Mzingile pia katika riwaya ya Bina
– Adamu.Mwandishi wa riwaya ya Mzingile
ameweza kuonesha matabaka ya kisiasa, kiuchumi hata kijamii. Mfano, msanii
anaonesha tabaka la kisiasa kupitia kwa mhusika kipofu, ambaye ni tabaka tawaliwa lisilomiliki chochote na ambalo
halina sauti juu ya tabaka tawala, halikadhalika Kipofu anatumika kama tabaka
tawaliwa lisilo na elimu linaloongozwa na tabaka tawala lenye elimu (uk. 28)
ambapo hadhira (watazamaji) wamekaa kulingana na hadhi zao. Mwandishi anaonesha
jinsi tabaka tawala wanavyotumia mali kwa mambo ya starehe bila kujali wala
kuwasaidia tabaka tawaliwa kwa kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Katika (uk. 45) mwandishi anasema,
“Katika mstari wa mbele kabisa
walikuwa wamekaa wanasiasa mashuhuri kutoka nchi
mbalimbali kama kawaida yao hawakupenda kuona mtu mwingine mbele yao. Viti
vyao vilikuwa vya starehe zaidi. Walikuwa viongozi na walipaswa kuongoza
katika
kuona. Nyuma yao walifuatia viongozi wa dini mbalimbali.”
Pia
katika riwaya ya Bina-Adam matabaka
yamejitokeza kama ya kisiasa, kiuchumi,
na kijamii.Pia utabaka katika jamii zetu limekuwa tatizo kubwa kwani tunaona
viongozi wanajilimbikizia madaraka na kuwakandamiza wanyonge. Seuze ya hayo
katika jamii yapo matabaka kati ya wenye navyo na wasio navyo, wasomi na wasio
soma na madhara ya matabaka katika jamii yanaleta utengano baina ya wanajamii
jambo ambalo sio zuri.
Usihiri,
haya ni mambo ya ajabuajabu yasiyoweza kuthibitika na ambayo yapo kinyume na
mambo ya uhalisia wa jamii. Katika
riwaya ya Mzingile usihiri umeweza
kujitokeza kwa namna mbalimbali. Mfano usihiri juu ya kuzaliwa na kukua kwa Kakulu, mwandishi anaonesha jinsi Kakulu
anavyozaliwa akiwa mtu mzima, mwenye ndevu, badala ya kunyonya anataka ubuyu na
kitendo cha kuongea akiwa tumboni kama inavyothibitika katika (uk. 1),
mwandishi anasema,
“Wanakijiji walimpa jina la
Kakulu kwa sababu alizaliwa akiwa na
ndevu tayari- Kakulu, kakubwa, kazee! Habari zilivuma kwamba
hakupata kunyonya ziwa la mama yake. Siku hiyohiyo aliyozaliwa, alimwomba
mama yake ubuyu ulioivia mtini.”
Halikadhalika
suala la usihiri linajitokeza kwenye chemichemi, sehemu ambayo kichaa pamoja na
kundi kubwa la watu wanapooga maji ya mvua na kujikuta wakibanduka na kubaki
mifupa tu kisha wanakimbiana. Katika (uk. 20), mwandishi anasema,
“Nilipojaribu kujisugua mwili
nilibandua ngozi na nyama yake mifupa ya mikono
yangu
ilianza kuonekana sote tulikuwa mifupa iliyosimama na kutembea.”
Pia
suala la usihiri limeonekana katika riwaya ya Bina - Adamu! ambapo wakati mwandishi ametumia wahusika wa ajabu
ajabu mfano, Hanna ambaye alikuwa anabadilikabadilika mara kwa mara anafanana
na watu mbalimbali.
Suala
la usihiri kama alivyotumia mwandishi kwenye kazi yake ya Mzingile na Bina- Adamu!
pia lina uhalisia katika jamii tunayoishi ikizingatiwa kuwa, kuna masuala ya
ushirikina na uchawi mambo ambayo
yanayohusiana na kuwafanya watu misukule
ambao huwa hawaonekani katika macho ya kawaida ya binadamu. Pia usihiri
hujitokeza katika jamii wananchi ambao wana migogoro ya nafsi kwani mgogoro
ukikomaa mwishoni wanauana. Mfano, wanaua watoto waopamoja na ndugu zao.
Usihiri
pia, unajidhihirisha katika jamii yetu ya sasa kwani,kuna mambo ya ajabu ajabu
yanayojitokeza katika jamii yetu tuliyomo. Kwa mfano, wanajamii kusafiri kwa ungo,
kusafiri kwa kumtumia myama fisi, pia kuwaroga watu usiku wakiwa wamelala.
Kwa
kuhitimisha, tunaweza kusema kuwa riwaya ya Bina
-Adamu inasawiri maisha na hali halisi ya kiafrika na dunia kwa ujumla. Kwa
mfano, sera ya dunia ambayo ni utandawazi imeelezewa kwa urefu na undani zaidi
kwa kuonyesha madhara yake katika nchi
zilizoendelea na zinazoendelea.Vilevile inasawiri hali halisi kwa sababu katika
jamii za kiafrika kuna watu ambao wanatafuta suluhisho kama ambavyo mhusika
mkuu Mimi, ambaye alisafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani kutafuta ufumbuzi
juu ya maisha ya watu wa nchi za kiafrika. Hivyo nchi za kiafrika zikijaribu
kutatua matatizo kwa mbinu tajwa kama ubaguzi wa rangi, ukabila na kufanya vitu
vionekane kwa uhalisia wake (ukengeushi), zinaweza kupambana na matatizo
mbalimbali.
MAREJELEO
12-07-wamitila- 1-pdf,Swahili forum (2005):95-97, mahojiano mafupi na cutz diegner juu ya
riwaya
ya Bina –Adamu.
Florence L. V. (2013), Sifa za uhalisia ajabu na umuhimu wake katika utenzi wa mwana
Fatuma:
tasnifu; chuo kikuu cha Nairobi.
Madumula J.S, (2009), Riwaya ya Kiswahili historia na misingi ya uchambuzi. NAIROBI:
Sitima printer and
station ltd.
Muhando P.Balisidya (996), Fasihi sanaa za maonyesho. Dar es salaam Tanzania publishing
house.
Nkwera, F.V (1978), Sarufi na fasihi Sekondari na vyuo. Dar-es-salaam Tanzania
Publishing
house.
Wamitila, K.W (2003), Kamusi ya fasihi, istilahi na nadharia.
www.GAFKO
SOFT.com/swa/Riwaya 2009-2004
ANGALIZO: MAKOSA YALIYOJITOKEZA KATIKA MAKALA HII NI YA KIUCHAPAJI NA SIO YA VYANZO REJEWA HAPO JUU.
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni