Ijumaa, 29 Aprili 2022

 MAANA NA NADHARIA YA UHALISIA MAZINGAOMBWE

     Na Kagita

     Baadhi ya wahakiki kama vile Abrams, wanadai kwamba uhalisiamazingaombwe kama dhana au istilahi imeanza katika miaka ya 1920. Kuambatana na hilo, kwa mfano, Shannin Schroeder anadai kwamba Mjerumani Franz Roh ndiye aliyevumbua matumizi ya 'Magischer Realismus' mnamo 1925 (katika kazi yake juu ya mtindo wa sanaa ya kisasa ya Ulaya enzi zile;  Usemi wa Kijerumani ambao ndio msingi wa 'Magical Realism' ya Kiingereza na 'uhalisiamazingaombwe' kama tunavyosema kwa Kiswahili siku hizi .(Schroeder 2004: 2).

 Theo D’Haen alimuunga mkono kuwa  Roh alikuwa mwasisi wa tamko la uhalisiamazingaombwe ambapo Roh alisema kuwa neno hili lilimaanisha, kuelekezea michoro iliyo na uhalisia kama wa picha ya kamera lakini ambayo iliibua hisia za kutokuwa halisi kwa kuchanganya uhalisia na ukosefu wa uhalisia.

D’Haen( 2005: 191). Ameeleza uhalisia mazingaombwe ni tawi mahsusi la usasa baadaye (postmodernism), linaonesha sifa za kujirejelearejelea, uziada uliopindukia, uanuwai, mseto wa vitu, mwingiliano matini, kuchezea na kuyumbisha uthabiti wa wahusika na usimulizi vilevile, kumchanganya msomaji kwa makusudi na halikadhalika kufuta mipaka kati ya dhana, vitu, au hali tofauti.

Warnes( 2002: 488). Anadai kuwa hoja kwamba Roh ndiye mwasisi wa uhalisiamazingaombwe ilipingwa au kurekebishwa na wahakiki kama vile Christopher Warnes anayedai kwamba matumizi ya awali kabisa ya istilahi ya 'uhalisiamazingaombwe' yanapatikana katika maandishi ya mshairi Friedrich Freiherr von Hardenberg, maarufu kwa lakabu ya kishairi Novalis (1772- 1801).Hata hivyo  Novalis hakuikuza mno dhana ya uhalisiamazingaombwe pamoja na kwamba alikuwa wa kwanza kuitumia. Labda ndio sababu wengi humtaja Franz Roh aliyetumia kinadharia kauli ya uhalisiamazingaombwe mwaka  1925 kama mwasisi wa istilahi hii. 

Mathew J. A. Green (2009) anasisitiza kwamba yamkini mitindo na misingi ya uhalisia mazingaombwe katika fasihi kimatendo ilikuwa ya awali zaidi hasa katika kaida za Kiramsia (Romanticism) ambapo masimulizi “yaliyaweka sambamba matukio ya kiajabuajabu na yale ya kawaida” 

.(Schroeder 2004: 2) Aidha baada ya Novalis and Roh walitokea wengine waliopanua matumizi na kukuza maana. Mathalani pale ambapo Roh alitumia uhalisiamazingaombwe kurejelea sanaa ya uchoraji tu, Mwitaliano Massimo Bontempeli alikuwa wa kwanza kuitumia istilahi hiyo kwa ajili ya “sanaa na fasihi”.

  Zamora & Faris (2005: 5).    wanapodai kwamba “uhalisia mazingaombwe unaafiki kutalii—na kukaidi—mipaka, si hoja kama mipaka hiyo ni ya kiontolojia, kisiasa, kijiografia, au kiutanzu” 

Kwa ujumla, uhalisiamazingaombwe  ni  mkabala wa kuuwakilisha uhalisia kwa kukiuka mipaka, kuhujumu au kuvuruga usimulizi mbali na kukaidi kaida za lugha. 



 UHALISIA MAZINGAOMBWE KATIKA FASIHI YA KISWAHILI

Kyallo W. Wamitila katika makala yake ya 1999, 'Influence or Intertextuality? A Comparative Study of Kezilahabi’s Nagona and Mzingile and Juan Rulfo’s Pedro Paramo', anabainisha jinsi fasihi ya Kiswahili inavyotoa mwangwi wa fasihi ya Amerika Kusini kwa kufumbata sifa za uhalisia mazingaombwe. Hii ni mojawapo ya makala za kwanza kabisa kugusia uhusiano huu wa kimtindo kati ya fasihi ya Afrika Mashariki ya tapo hili na kwengineko.

 Na ingawa inaweza kudaiwa kwamba kazi za Shaaban bin Robert kama vile Kusadikika (1951) na Kufikirika (1946/1967) zilikuwa na sifa fulani za uhalisiamazingaombwe, Wamitila anasisitiza mchango mkubwa wa Euphrase Kezilahabi katika kuleta upya katika ulingo wa fasihi ya Kiswahili. 

UDHAIFU WA UHALISIA MAZINGAOMBWE KATIKA KAZI ZA FASIHI

Kuhusisha wahusika wakuu walio na akili zisizo timamu, mwingiliano-matini uliopindukia na utambulisho wenye kutetereka.

Umefungwa kwa minyororo ya lugha, na hivyo basi hauwezi kuondoa udhaifu wa lugha katika kuweza kuwakilisha hali halisi kikamilifu. 


 MAREJELEO.

Abrams, Meyer H.(1999). A Glossary of Literary Terms. Ithaca:  Cornell University Press. Benyei,

 Tamas. (1997). Rereading ‘Magic Realism’. Hungarian Journal of English and Ameri- can Studies 3/1: 149-179.

 Cooper, Brenda. (1998). Magical Realism in West African Literature: Seeing with a Third Eye. New York: Routledge. 

Camus, Albert. (1948). The Plague. Tafsiri ya Stuart Gilbert. New York: Modern Library.

 D’Haen, Theo L. (2005). Magic realism and Postmodernism: Decentering Privileged Centers. 

 Zamora Lois Parkison & Wendy Faris (Eds.) Magic Realism: Theory, History, Community. Durham & London: Duke University Press. pp. 191-208.