DHANA YA MOFOLOJIA, MOFOFONOLOJIA NA MICHAKATO YA KIMOFOFONOLOJIA
Na Mwl. Kagita I.S.A
Katika makala hii nitaanza kueleza maana ya fonolojia, mofolojia na mofofonolojia kwa kutalii wataalamu mbalimbali, kisha nitaeleza michakato ya kimofofonolojia nikijigeza katika mawazo ya wataalamu tofautitofauti.
Wataalamu
mbalimbali wamefasili fonolojia na mofofonoloji kama ifuatavyo;
Kwa
mujibu wa Mugulu (1999), akimrejelea Fudge (1973) anasema kwamba fonolojia ni
kiwango kimojawapo cha lugha fulani kilicho na vipashio vidogo zaidi kuliko
vipashio vingine vyote vya lugha. Vipashio vya kifonolojiani fonimu na alofoni
zake.
Dosari
ya fasili hii ni kwamba haijafafanua kiwango kipi cha lugha ambacho kinahusika
na fonolojia kwani lugha inaviwango mbalimbali.
Massamba
(2010) anasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na mfumo wa
sauti (asilia) za lugha. Hii inamaana kwamba, kila lugha mahususi inamfumo wake
wa sauti ambamo maneno hujengwa. Ki ukweli fonolojia hujihusisha na namna sauti
zinavyotumika katika maneno ya lugha mahususi katika kuleta maana.
Massamba na wenzake (2004)
wanafafanua kuwa, fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughusha na uchunguzi,
uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo
mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu.
John Habwe na Peter Karanja (2004)
wanaeleza kuwa; fonolojia ni utanzu wa isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha
zinavyofanya kazi katika lugha mbalimbali. Fonolojia huchunguza jinsi sauti
hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi
ili kuunda tungo zenye maana.
Pia maana ya mofofonolojia imeelezwa
kama ifuatavyo;
Massamba (2010) akimnukuu Martinet
(1965) ambapo Martinet alinukuu kutoka kwa Trubetzkoy (1929) anaeleza kuwa;
mofofonolojia kama ilivyotumiwa na Trubetzkoy ilimaanisha sehemu ya isimu
ambayo ingeweza kutumia mofolojia kuelezea tofauti fulani za kifonolojia ambazo
zisingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia peke yake.
Dhana
ya michakato ya fonolojia na mofofonolojia imejadiliwa na wataalam mbalimbali
kama ifuatavyo;
Tuki
(2004) inaeleza kuwa mchakato ni mfululizo wa shughuli unaosababisha kitu
fulani kufikiwa.
Hivyo
katika uwanja huu wa fonolojia tunaweza kusema kuwa mchakato utakuwa
unafanyika pale ambapo mofimu mbili zinapokutanishwa huweza kutokeza mabadiliko
fulani katika mofimu mojawapo au kutotokea badiliko lolote. Mfano viungu
hubadilikia kuwa vyungu,kietu hubadilika kuwa chetu hapa tunaona kuwa
mabadiliko yametokea lakini miti hubakia kuwa miti, kiti hubakia kuwa kiti na
hapa tunaona kuwa hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea.
Massamba
(2011) anaeleza kuwa kuna aina mbili za michakato asilia yaani mchakato
usilimisho na mchakato sio-usilimisho. Mchakato wa kiusimilisho anasema kuwa,
usilimisho ni pale ambapo kitamkwa kimoja hufanywa kifanane na kitamkwa kilicho
jirani yake kwa maana kwamba hupata baadhi ya sifa za kipande sauti chenziye
kilicho jirani. Kwa mfano, konsonanti inaweza kupata baadhi ya sifa za irabu au
irabu ikapata baadhi ya sifa za konsonanti, na konsonanti moja huweza kuathiri
konsonanti nyenziye au irabu moja huweza kuathiri irabu nyenziye. Pia
anaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha michakato kadhaa kama
vile,unazalishaji wa irabu, utamkiaji pamwe wa nazali, ukaakaishaji,
ughunishaji kati irabu, uhafifishaji kati irabu, tangamano la irabu,
ughunishaji konsonanti shadda, muungano.
Pia,Habwe
na Karanja (2004), wanaeleza kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa
kiasi au kikamilifu kutokana na kuathiriana. Hapa sauti jirani katika neno
huathiriana kiasi kwamba fonimu hupokea ama kupoteza sifa za kifonetiki kwa
fonimu jirani, na matokeo yakiwa kuwa fonimu hizi hukabiliana sana katika
kufanana. Pia wanaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha kuimarika,
kodhoofika, kuingizwa, kudondoshwa, au kuungana kwa fonimu katika neno.
Hivyo
basi katika mchakato huu wa usilimishaji tunapata aina kuu mbili za
usilimishaji kama zifuatazo;
Usimilisho wa nazali; ni aina ya usilimisho ambao nazali huathiriwa na konsonanti inayofuatana
nayo hivyo nazali inasimilishwa yaani hutamkiwa mahali pale ambapo konsonanti
inatamkiwa. Kwa mfano nazali zote hutumia msimbo “N”
Kwa hiyo, [ l ] [ d ] N-
[ r ]
[ d ] N-
Hivyo basi, fonimu konsonanti / l /
na / r / zinzpokzribiznz nz irabu haziathiriki lakini zinapotanguliwa na / n /
hubadillika na kuwa / d / na zote hutamkiwa kwenye ufizi.
.Mfano
umbo la ndani
|
umbo la nje
|
/n+buzi/
|
[mbuzi]
|
/n+bwa/
|
[mbwa]
|
/n+bu/
|
[mbu]
|
/n+gongo/
|
[mgo go]
|
/n+gozi/
|
[ gozi]
|
/n+vua/
|
[ vua]
|
/n+vivu/
|
[ vivu]
|
Usilimisho wa Konsonanti ni aina ya usilimisho ambao konsonanti huathiriwa na nazali inayofuatana
nayo hivyo konsonanti inasimilishwa yaani hutamkiwa mahali pale ambapo nazali
inatamkiwa. kuna baadhi ya sauti ambazo huathiriwa na nazali “n” inapokuwa
inaandamia yaani kuna sauti ambazo huathiriwa zinapokaribiana au karibiana moja
kwa moja na nazali “n”. mara nyingi hutokea katika maumbo ya umoja na uwingi
katika maumbo ya maneno
Mfano:-
Umbo la nje
|
umbo la ndani
|
Ulimi
|
u+limi
|
Ndimi
|
u+limi
|
Urefu
|
u+refu
|
Ndefu
|
n+defu
|
Kwa hiyo kama vile ulimi mrefu
|
Ndimi ndefu
|
Hapa
tunaona kwamba sauti [ l ] na [ r ] zinapokaribiana na irabu na irabu
haziathiriki lakini zinapokaribiana na nazali “n” hubadilika na kuwa “d”
Kanunixxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Pia kuna michakato isiyo ya kiusimilishokama
ifuatayo;
Uyeyushaji
Uyeyushaji,
wataalamu wengine huita irabu kuwa nusu irabu Mgullu (1999). Huu ni mchakato
ambapo irabu irabu za juu /u/ na /i/ hubadlika na kuwa /w/ au / j/ katika
mazingira ya kufuatiwa na irabu zisizofana nazo. Kwa kifupi ni kwamba /u/
inapofuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika kuwa [w] na /i/
ikifuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika na kuwa [j].
Hivyo
uyeyushaji ni kanuni inayoelezea mabadiliko ya sauti (irabu) na kuwa kiyeyusho
aidha [w] au [j] hii ni kwa irabu zote za juu zinapofuatana na sauti zingine
zisizofanana nazo. Na sauti hizo hubadilika katika mazingira ya /u/ hubadilika
kuwa [w] inapofuatana na irabu nyingine isiyofanana nayo na / i/ inabadilika na
kuwa [ϳ] pia inapofuatana na irabu isiyofanana nayo.
Mfano
wa /u/
umbo
la ndani
|
umbo
la nje
|
/mu+aminifu/
|
[mwe:mbamba]
|
/ku+enu/
|
[kwe:nu]
|
/mu+
anafunzi/
|
[mwa:nafunzi]
|
/mu+eupe/
|
[mwe:upe]
|
/mu+embe/
|
[mwe:mbe]
|
Kanuni
/u/ [w]
I [-u]
Hivyo
tunaona wazi kabisa kuwa irabu ya juu nyuma /u/ imebadilika na kuwa
kiyeyusho [w] katika mazingira ya kuatiwa na irabu isiyofanana nayo
ambayo ni /a/ na /e/ kwa hapo juu lakini hata ikiwa ni /o/ huweza
kubadilisha.
Mfano
wa irabu /i/
/umbo
la ndani/
|
[umbo
la nje]
|
/mi+embe/
|
[mje:mbe]
|
/mi+endo/
|
[mje:ndo]
|
/mi+ezi/
|
[mje:zi]
|
/mi+anzo/
|
[mja:nzo]
|
/mi+eusi/
|
[mwe:usi]
|
/mi+oyo/
|
[mjo:jo]
|
Kanuni; /i/ /j/
I [-i]
Hivyo
tunaona kuwa irabu ya juu mbele /i/ hubadilika na kuwa [j] inapofuatana na irabu
nyingine isiyofanana nayo ambayo ni /e,a na o/.
Ukaakaishaji
Mgullu
(1999) akimnukuu Les (1984), anadai kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea ambapo
fonimu zisizo za kaakagumu zinapobadilika na kuwa za kaakagumu. Katika
Kiswahili sauti za kaakagumu zipo mbili tu yaani /ɟ/ na /ʧ/ ambazo ni vizuiwa
kwamizwa. Anamalizia kwa kusema kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea wakati
ambapo fonimu zisizo vizuiwa kwamizi hubadilika na kuwa vizuiwa kwamizwa. Hii
katika ukokotozi wake unakuwa kama ifuatavyo.
umbo
la ndani
|
umbo
la nje
|
umbo
la nje
|
/ki+enu/
|
[kjenui]
|
[
enu]
|
/ki+eusi/
|
[kjeusi]
|
[
eusi]
|
/ki+ombo/
|
[kjombo]
|
[
ombo]
|
/ki+umba/
|
[kjumba]
|
[
umba]
|
/ambaki+o/
|
[ambakjo]
|
[ambao]
|
Kanuni; /k/ /ʧ/ /j/
Hapa tunaona kwamba kipasuo cha
kaakaalaini /k/ hubadili mahali pa matamshi na kuwa kizuiwa kwamizi /ʧ/ cha
kaakaagumu katika mazingira ya kufuatiwa na sauti /ϳ/.
Tangamano
la irabu.
Huu
ni mchakato ambao irabu fulani hukubali kuandamana katika mazingira maalumu.
Kwa mfano mofu [i] na [e] katika lugha ya Kiswahili huonekana kama alomofu au
maumbo mbalimbali ya mofu moja ya kutendea na kutendesha, lakini utokeaji wake
hutegemeana na mofu itakayojitokeza katika mzizi. Kama irabu ya mzizi ni
/i/, /u/ au /a/ basi irabu ya kiambishi cha utendea lazima kiwe ni [i] ,
wakati irabu ya mzizi ikiwa ni /e/ au /o/ katika hali ya utendea
kiambishi chake kitakuwa ni [e]. Mfano.
umbo
la ndani
|
umbo
la nje
|
/imb+a/
|
[Imb-i-a]
|
/andik+a/
|
[andik-i-a]
|
/dak+a/
|
[dak-i-a]
|
/chun+a/
|
[
un-i-a]
|
/og+a/
|
[og-e-a]
|
/
ez+a/
|
[
ez-e-a]
|
/kom+a/
|
[kom-e-a]
|
Kanuni;xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Hapa
mofimu ya utendea ina alomofu mbili ambazo ni /i/ na /e/ ambapo alomofu /i/, inatokea
pale ambapo irabu ya mzizi inakuwa na /i/,/u/ na /a/ wakati ambapo alomofu /e/
inatokea wakati irabu ya mzizi ikiwa ni /e/ na /o/.Kinachoonekana hapa ni
kwamba irabu zinatangamana kwa kufuata mahali pa matamshi. Kwa mfano kama irabu
ya mzizi ni ya juu basi irabu ya utendea pia itakuwa ni ya juu, na irabu ya
mzizi ikiwa ni ya kati basi irabu ya utendea pia itakuwa ya kati,na irabu ya
chini siku zote inaonekana kuwa ni ya juu.
Udondoshaji, kanuni hii inahusu kuachwa kwa sauti fulani katika matamshi
wakati mofimu mbili zinapokaribiana yaani katika mazingira hayo hayo ya sauti
ambayo ilikuwepo hapo awali hutoweka.hapa kuangalia umbo la ndani la neno na umbo la nje.
Kwa mfano irabu /u/ ikifuatiwa na
konsonanti halisi basi irabu hiyo hudondoshwa, kama inavyooneshwa hapa chini.
umbo la ndani
umbo la nje
Muguu mguu
Mutu mtu
Mujapani mjapani
Musichana msichana
Kanuni; /u/ Ø k[halisi]
Mara nyingi irabu “u” katika mofimu
“mu” ikabilianapo na na mofimu fulani
hasa konsonati halisi katika mpaka wa mofimu, irabu “u” hudondoshwa lakini
inapokabiliana na irabu inayofanana nayo hubaki kama ilivyo.
Mfano; Muumba- muumba
Muumini- muumini
Muuguzi-muuguzi
Muungwana- muungwana
Pia
udondoshaji hutokea pale ambapo irabu mbili zinapofuatana katika mpaka wa
mofimu, kwa mfano
Umbo
la ndani
Umbo la nje
Zietu
zetu
Hautaki hutaki
Chaake
chake
Kanuni; /I/1 Ø /I/2
Yaani irabu ya kwanza inadondoshwa
katika mazingira ya irabu hiyo kufuatiwa na irabu ya pili.
Muungano wa irabu, kanuni hii hutokea pale ambapo irabu ya mofimu moja
inapokabiliana na irabu ya mofimu nyingine katika mpaka wa mofimu irabu hizo
huungana na kuzaa irabu moja, na irabu hizo sharti moja iwe ya chini na nyingine ya juu.
Mfano;
Umbo la ndani
|
Umbo la nje
|
Wa
+ enya
|
wenye
|
Wa
+ ingi
|
wengi
|
Ma
+ ino
|
meno
|
Wa
+ izi
|
wezi
|
Wa
+ enzi
|
wenzi
|
Ma+ino
|
Meno
|
Wa+izi
|
wezi
|
Kanuni; /a+i/=e mpakani mwa mofimu.
Lakini
kanuni hii haifanyi kazi wakati wote kwani kuna mazingira mengine ambayo
haifuati hasa katika mofimu mnyambuliko
Mfano:-
Wa
+ igizi +a +ji - waigizaji
|
Wa+ingereza -
waingereza
|
Wa +oko+a+ji - waokoaji
|
Wa+ite - waite
|
Mwisho, taaluma ya mofolojia na fonolojia licha ya kuwa na uhusiano mkubwa kupitia athari zilizojadiliwa hapo awali, taaluma hizi zina usigano mkubwa hii ni kwa sababu fonolojia inajishughulisha na uchambuzi na ufafanuzi wa sauti za lugha mahususi lakini fonolojia inahusika na uchambuzi wa maumbo ya sauti (maneno) bila kujali kuwa ni ya lugha mahususi au laa!.
MAREJEO
Habwe,
J na Peter K. (2004) Misingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix
Publishers:
Nairobi.
Massamba,D.P.B.
(2011) Maendeleo Katika Nadharia ya Fonolojia. Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili (TUKI): Dar es Salaam.
Mgullu,
R.S. (1999) Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili.
Longhorn Publishers
Ltd: Nairobi
TUKI, (2004) Kamusi ya Kiswahili
Sanifu. Oxford University Press: Nairobi.
TANBIHI; Ikumbukwe kuwa makosa ya kiuandishi yatakayojitokeza katika makala hii hayana uhusiano wowote na vyanzo rejewa hapo juu.
imekaa poa,kazi nzuri
JibuFuta