Katika makala hii tumeanza kwa kueleza dhana ya fani kisha tukatazama maana ya tamthiliya kulingana na wanazuoni mbalimbali, kisha tukagusia chimbuko na maendeleo ya tamthiliya kwa kifupi na mwisho tumejadili vipengele mhimu vya fani katika tamthiliya ya Kivuli Kinaishi iliyoandikwa na Said Mohamed.
Kwa kuanza na dhana
ya fani.
Fani
ni ufundi katika kuumba umbo la kazi ya fasihi kutokana na ubunifu wake. Fani
hujuisha muundo, mtindo, matumiziya lugha wahusika na mandhari (www.mwanchi.co.tz/makala/vipengele
mhimu vya uhakiki wa kazi ya fasihi).
Fani
ni ufundi wa kisanaa anaoutumia msanii katika kazi yake. Ni ustadi au ubingwa au
mbinu ambazo msanii wa kazi ya fasihi hutumia katika kuwasilisha ujumbe wake
kwa hadhira yake.(Senkoro 1982:8)
Fani
ni sanaa, ni jumla ya vipengele vya lugha vilivyowekwa katika mpangilio
mahususi ili kutoa kwetu maana Fulani (Mulokozi na Kahigi 1978:53).
Kwa
ujumla, fani ufundi au ujuzi wa kisanaa atumiao mwandishi au mtunzi wa fasihi
katika kufikisha ujumbe kwa jamii/hadhira iliyokusudiwa. Fani ni kipengele
pekee ambacho humtofautisha kati ya msanii mmoja na mwingine, mfano wa
vipengele hivyo ni matumizi ya lugha, mtindo, muundo, mandhari, na hata ujuzi
wa wahusika.
Tamthiliya
ni mchezo wa kuigiza au utungo wa kisanaa ambacho huweka wazo Fulani katika
matendo na mazungumzo (Nkwera h.t.chombez.blogsport.com/2013/11/tmthiliya.htm/?.m=1)
Tamthiliya
ni utungo wa kisanaa ambao huweka wazo Fulani katika matendo na mazungumzo
(Tuki 2004).
Tamthiliya
ni utungo wa fasihi ambao hubuniwa, kwa kiasi kikubwa kwa lugha ya mazungumzo
yenye kuzua na kuendeleza matukio ya hadithi ya utungo huo. Chanzo cha matukio
ya hadithi ya tamthiliya mara nyingi hupatikana humohumo katika mazungumzo ya
wahusika wake (Mazrui na symbo 1992).
Mlokozi (1996) anasema hadithi ya tamthiliya husonga mbele kwa njia ya vitendo
na mazungumzo ya wahusika. Hivyo anaonyesha bila wahusika hata mazungumzo
hayatakuwepo. (chombez.blogspot.com/2013-11-01-achieve).
Kwa
ujumla, tamthiliya ni andiko la kiuigizaji linalotoa simulizi kwa kuonyesha
maneno na matendo. Hii inamaana kwamba tamthiliya ni utanzu ambao hauna
msisitizo wa kuigizwa jukwaani ukilinganisha na drama na pia tamthiliya lazima
ikidhi vigezo vya kidrama kwasababu isipokidhi inakuwa chapwa yaani haina
shauku. Vigezo vya kidrama ni kama vile muonekano dhahiri wa jukwaani, mwonekano
dhahiri wa hisia, usikiaji wa ngoma, ishara na matendo, ushiriki wa moja kwa
moja wa hadhira na usikiaji dhahiri wa sauti za binadamu, ndege au wanyama.
Fasihi
ya majaribio au tamthiliya ya majaribio ni fasihi iliyo lenga kuleta upya
katika fasihi ya Kiswahili. Watunzi wengi wa tamthiliya ya Kiswahili walikuwa wakitunga
kazi zao kwa kuiga mbinu mbinu na kanuni za tamthiliya ya ulaya. Kuanzia miaka
ya 1970 watunzi wa tamthiliya ya Kiswahili hawakuridhika na uigaji huo. Waliona
kuwa kuna umuhimu wa waafrika kuwa naTamthiliya yao yenye kuchota mbinu zake
kutokana na sanaa za jadi za kiafrika. Lengo kubwa lilikuwa nikufanya Tamthiliya
ioane na utamaduni na mazingira ya kiafrika(Mlokozi 1996).
Kwa
mjibu wa Senkoro (2011:62-63) anaeleza kuwa majaribio mengi yanayofanyika
katika Fasihi ya Kiswahili yanaelekea kuwa yamechota kutoka katika fasihi
simulizi ya Kiswahili.
Kwa
ujumla, Tamthiliya ya majaribio ni aina ya Tamthiliya ambayo hutumia mbinu na
taratibu ambazo hazijazoeleka katika kumbo la kawaida la Tamthiliya, hii
inamaana kwamba vipengele mbalimbali vya fani na maudhui ambavyo vilichukuliwa kutoka
katika fasihi simulizi vikaingizwa katika tamthiliya ya Kiswahili ya majaribio
ili kuonyesha utofauti uliopo kati ya Tamthiliya ya kiafrika na kimagharibi.
Hapo
mwanzo kabla ya kuibuka kwa Tamthiliya ya Kiswahili ya majaribio hapa kwetu
Afrika kulikuwa aina tofauti za sanaa za maonyesho kama vile utambaji, ngoma,
miviga na sherehe ambazo zilikuwa na sifa zifuatazo: Zilitungwa hapo hapo,
hazikuandikwa, hazikuwa za biashara, zilifanywa kwenye duara, hadhira na
watendaji walibadilishana nafasi na sanaa iliyokamilika haikuwa ya mtu mmoja
bali ya jamii nzima.
Baada
ya ujio wa tamthiliya za kimagharibi umbo lake lilitofautiana na sanaa za
maonyesho za asili kwani zilikuwa na mambo yafuatayo: Maandishi, waigizaji,
hadhira, ukumbi, jukwaa, matapo, mgawanyo dhahiri wa majukumu(kazi), zilikuwa
za biasharana zilikuwa mali ya mtu mzima. Hivyo waandishi wengi wazawa walianza
kuandika kazi zao za tamhiliya kwa kufuata kanuni za uandishi wa kiaristotle.
Kuanzia
miaka 1970 watunzi wa tamhiliya ya Kiswahili hawakuridhika na uigaji wa
tamthiliya za kimagharibi(kiaristotle). Hivyo waliona kuwa kuna umuhim wa
waafrika kuwa na tamthiliya yao yenye kuchota mbinu zake kutoka katika sanaa za
jadi za Kiafrika. Lengo kubwa ilikuwa ni kuifanya tamthiliya ioane na utamaduni
na mazingira ya kiafrika.(Mulokozi 1996).
Kwa
kutumia mifano kutoka katika Tamthiliya ya KIVULI KINAISHI ya Said Mohamed vipengele mhimu vya kifani vinavyojitokeza
katika tamthiliya ya Kiswahili ya majaribio ni kama vifuatavyo:
Mtindo, ni jumla ya mbinu au sifa
zinazomwezesha msanii kuwasilisha ujumbe wake au kuelezea msanii anavyounda
kazi yake(Wamitila 2003). Katika kipengele hiki cha mtindo wasanii wengi wa
tamthiliya ya Kiswahili ya majaribio huchanganya tanzu mbalimbali za kisanna
kama vile nyimbi, ushairi na hadithi. Mfano, katika tamthiliya ya KIVULI KINAISHI iliyoandikwa na
Said Mohamed imechanganya tanzu mbalimbali kama nyimbo na hadithi. Mfano katika
onyesho la nne.(uk.31) mwandishi ametumia wimbo anasema;
“NYIMBO: Nasikia parakacha myembeni
Kam
mshambigija mleteni
Eee wewe … eee wewe
Kupeana ni kikoa,
Toa name nitoe
Ati kupeana ni kikoa
Toa name n’toe!”
Utanzu mwingine alioutumia katika Tamthiliya
hii ni hadithi mfano katika onyesho la kwanza (Uk10) msanii anasema ;
“Bi.kizee; Haya(anaingia hadhira huku anavuta ugoro na
huku
anapakasa ukili wake- kaketi kijamvini)
paukwaa….
Wtoto na
hadhira: kimya
Bi. Kizee: paukwa…….
Watoto na
hadhira; kimya
Bi.
Kizee: paukwa…itikieni….itikieni basi….
Watoto na
hadhira; Pakawa….”
Kwa
hiyo mbinu hii ya kuchanganya tanzu katika kazi moja ya fasihi husaidia hadhira
kuvutiwa na kuhamasisha kwa wasomaji kutokana na kuoana na utamaduni wao.
Vilevile
methali zimeweza kujitokeza katika( Uk.24) anasema,
“unachumia juani na kulia kivulini, (Uk.67)
kikulacho kinguoni mwako, (Uk.111) majuto ni mjukuu, (Uk.6) kuishi kwingi kuona mengi na kujua mengi pia”.
Muundo ni mpangilio wa kiiufundi
anaoutumia msanii katika kazi yake(Senkoro F.E.M.K(1982). Kwa ujumla muundo ni mpangilio
na mtiririko wa kazi ya fasihi simulizi kwa upande wa visa na matukio, muundo
hujumuisha jinsi msanii wa kazi ya fasihi alivyofuma, alivyounda na
anavyounganisha tukio moja na lingine, kitendo kimoja na kingine wazo na wazo,
sura moja na nyingine, ubeti na ubeti, hata mstari wa ubeti na mwingine. Mfano
katika tamthiliya hii ya KIVULI KINAISHI kuna visa viwili nadi ya kisa kimoja
yaani kisa cha Bi kizee na watoto na kisa cha maisha ya Giningi. Vilevile
mwandishi ametumia Mianzo na miishio ya kifomula mfano, mianzo ya kifomula(Uk10)
msanii anasema:
“Bi.kizee;
Haya(anaingia hadhira huku anavuta ugoro na
huku anapakasa ukili wake- kaketi
kijamvini) paukwaa….
Wtoto na
hadhira: kimya
Bi.
Kizee: paukwa…….
Watoto na
hadhira; kimya
Bi.
Kizee: paukwa…itikieni….itikieni basi…
Watoto na
hadhira: pakawa….”
Pia
ametumia miisho ya kifomula mfano, ukurasa wa mwisho kabisa (Uk130) onyesho la
10 mwandishi anasema;
“ Bi.kizee: Basi huo watoto ndio
mwisho wa hadithi…na kama mwisho wa hadithi ulivyo
Huwa furaha au
huzuni”
Kutokana na kipengele hiki cha mianzo na
miisho ya kifomula katika Tamthiliya ya kiswahili majaribio kimeleta upekee kwa
sababu huvuta umakini wa hadhira kuwa na shauku ya kutaka maudhui ya
Tamthiliya, na hii ni kutokana na maneno anayotumia msanii katika kuanza kazi
yake.
Matumizi ya lugha, ni namna ambayo
msanii ameteua na kupangilia tamathali za sema kama sitiari,tashbiha, takriri,
tashihisi, tafsida, methale, misemo, nahau, taswira na lugha za kigeni (Senkoro
F.E.M.K 1982). Katika Tamthiliya ya “KIVULI KINAISHI” iliyoandikwa na Said
Mohamed. Mwandishi ametumia taswira mbalimbali kama ifuatavyo: KIVULI KINAISHI
ni taswira inayo maanisha mawazo ya kimpinduzi yaliyokwisha pandikizwa na kwa
vizazi vipya ili kudai haki na usawa. Taswira nyingine ni “unga wa rutuba” (uk112)
yenye maana ya elimu ya kujitambua katika jamii na kutambua nafasi yako na kuwa
na uwezo wa kuwaelimisha wengine.
”Bi.kirembwe:
Enh! (anashituka….anashangaa) umebwia nini?
Mtolewa: unga wa rutuba…..
Bi.kirembwe: unga wa
rutuba……a-a-a-a-a-mbaya…..mbaya
Mtolewa: Ndiyo…………”
Taswira nyingine ni “unga wa ndere”
wenye maana ya itikadi zinazomfanya mtu katika tabaka tawala akubalike na
kushika miiko mfano (Uk.111) Mtolewa anasema:
“Mtolewa: Mtolewa wa leo hayupo
pamoja na wewe … yuko
maili
elfu na moja mbali na wewe. Mtolewa wa
leo
hasimamii mamlaka uliyompa, anasimamia
mamlaka
ya hawa wote waliopewa unga wa ndere..”
Taswira
nyingine ni mdundo wa ngoma unaomaanisha kitendo cha kufuata mashariti kama
tabaka tawala litakavyo (Uk.31) katika onyesho la nne.
“Kumbwaya,
ugoma maarufu wa Giningi, analia, kabla
pazia
kufunguliwa.Nyimbo nyimbo inakuja na ngoma inaimbwa
kwa sauti
za kike kwa kiume, za wakubwa kwa wadogo:
Pazia
linafunguliwa kidogokidogo kuwaridhisha wari
Wanaotaka
kuingizwa giningi.”
vilevile mwandishi ametumia takriri
katika onyesho la nane (uk.111) anasema,
Bi.kirembwe: “Ulumbi …ulumbi… uluumbi (anakwenda huku akirudi huku)
Umechomoka Mtolewa, majuto hakika ni mjukuu
nilihisi mimi
tokea mwanzo,lakini sijui kanini sikuchukua hatua?”
Hivyo kipengele hiki cha lugha katika Tamthiliya za kimajaribio kimeweza
kuleta upya katika kazi za fasihi kwa kuingiza vionjo asili vya kiutamaduni na kuepusha migogoro ya moja kwa moja kati
wasanii na tabaka tawala kwa kutumia lugha ya mficho kwa kutumia taswira.
Wahusika,
ni binadam wanaopatikana katika kazi ya fasihi ambao wana sifa za kimaadili,
tabia, kiitikadi na falsafa ambazo hutambulishwa na wanayoyasema na
wanayoyatenda.(Wamitila 2002). Katika tamthiliya wahusika hujidhihirisha katika
utambaji mfano, katika Tamthiliya ya KIVULI KINAISHI iliyoandikwa na Said Mohamed
amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashirikisha hadhira katika utambaji. Mfano
(Uk.60) onyesho la tano mwandishi anasema:
Mtangazaji:
Mpo? Wali mpo?
Wali
wote: tupooo!
Mtangazaji:
yote sawaaa?
Wali
wote: yote sawa…sawa….sawa…
Vilevile amefanikisha kuwashirikisha
hadhira (Uk10) msanii anasema,
Bi. Kizee: paukwa
Watoto na
Hadhira: Pakawa….
Hivyo basi ushirikishwaji wa hadhira ni
muhimu kwa sababu huipa Tamthiliya uhai, mvuto na kuondoa uchovu kwa hadhira.
Mandhari, ni sehemu ambayo matukio ya
hadithi au masimulizi hutokea.mandhari huweza kuwa halisi kama vile njiani,
msituni, kijini mjini au ya kufikirika kama vile kuzimu, peponi na mbinguni(Senkolo
F.EM.K.1982). Vilevile mandhari ni elementi ambayo hutufichulia wapi na lini
ambapo matukio Fulani yalifanyika(Wamitila 2002).mwandishi anaweza kutumia
mandhari halisi nay a kuonekana au mandhari ya kufikirika. Mfano katika
tamthiliya ya KIVULI KINAISHI mwandishi ametumia mandhari halisi ya kitanzania
kutokana na kutaja kwa miji kama vile unguja na pemba vile vile mambo kama
rushwa, uongozi mbaya na hali ngumu ya maisha vinaashiria nchi za dunia ya tatu
kama vile Tanzania ambapo baadhi ya viongozi hutumia madaraka yao vibaya.
Vilevile kuna mandhari ya kubuni katika onyesho la tisa (uk.117)mwandishi
anasema,
“BI
KIREMBWE: Na sauti hiyo inatoka wapi?
SAUTI:
Kuzimu…..
BI
KIREMBWE: Aha, sasa naanza kuelewa… sauti hiyo ni sauti ya Mtolewa
inayotoka kuzimu...”
Hivyo mandhari huifanya kazi ya fasihi
kuendana na uhalisia hasa mandhari halisi.
Kwa ujumla vipengele hivi ndivyo
hutofautisha Tamthiliya ya Kiswahili ya majaribio na kuipa upekee ukilinganisha
na Tamthiliya zilizotungwa kabla ya miaka 1970s ambazo zilikuwa na mlengo wa
Tamtiliya ya kimagharibi ambapo watunzi wa Tamthiliya hawakurithika na uigaji
huo, wakaona kunaumhimu wa waafrika kuwa na Tamthiliya yao yenye kuchota mbinu
zake kutokana na sanaa za jadi za kiafrika.
MAREJELEO
Faustine,
S. (2015) Tamthiliya ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma: (Hakijachapishwa.)
Mohamed,
S. (2009) Kivuli Kinaishi: Oxford University Press, East Africa ltd. Nairobi.
Mlokozi,
M.M (1996) Fasihi ya Kiswahili: Taasis ya Uchunguzi wa Kiswahili; Chuo Kikuu
cha Dar- es- Salaam.
nkwerah.t.chombozi.blogspot.com.n/2013/11/tamthiliya.htm/?.m=1
Nyangwine, N.& Masebo, J( 2007)
Fasihi kwa ujumla. Nyambari Nyangwine Publisher: Dar- es-Salaam.
TUKI
(2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu: Chuo Kikuu cha Dar-es- Salaam.
www.mwananchi.co.tz/makala/vipengele
muhimu vya uhakiki wa kazi ya fasihi.
Senkoro, F.E.M.K (2011) Fasihi Dar- es-
Salaam University Press: Dar- es- Salaam.
kazi nzuri sana hongera sana na endelea kufanya zaidi na zaidi
JibuFutaasante kwa kuturahisishia
JibuFutaasante
JibuFutaUko vizuri na nimekupata vizuri
JibuFuta